Home BIASHARA Mambo ya kuzingatia wakati unapanga bei

Mambo ya kuzingatia wakati unapanga bei

0 comment 135 views

Bei ni jambo muhimu katika biashara kwani  ni kichocheo kikubwa cha mafanikio. Wafanyabiashara wengi hupendelea kuiga mpangilio wa bei kutoka kwa washindani wao, au hufikiria bei inayowaridhisha na kuanza kuuza, jambo ambalo si sahihi na limewasababisha wengi kufunga biashara. Kama mfanyabiashara ni vyema ukazingatia mambo yafuatayo wakati wa kupanga bei ili kujihakikishia mafanikio na kupeuka hatari ya kupata hasara.

Soko

Kabla ya kupanga bei unatakiwa kufanya utafiti na kujua kama wateja wapo tayari kununua bidhaa au kupata huduma yako. Fanya utafiti na fahamu washindani wako wanatoza bei kiasi gani katika bidhaa au huduma husika. Baada ya kujua hayo, unaweza kuweka bei inayoendana na hiyo.

Gharama

Weka kumbukumbu ya gharama zote za moja kwa moja, pamoja na fedha zilizotumika kutengeneza bidhaa au huduma, kisha hesabu na gharama zilizotumika katika vifaa, ufungaji wa bidhaa nk halafu orodhesha na gharama za kudumu kama kodi na mishahara. Baada ya hapo, jumlisha kwa pamoja kisha jumlisha na asilimia ya kiwango cha tasnia ya rejareja (Markup) ili kupata bei, au kwa urahisi zaidi unaweza unaweza kuorodhesha gharama> kisha kujua thamani ya bidhaa husika> kujua wateja> na kuamua kuuza bidhaa kwa bei kubwa zaidi ya ile iliyopo sokoni (kwa lengo la kuonyesha jinsi bidhaa yako ilivyokuwa na thamani isiyo ya kawaida), au kuuza bei sawa na washindani wako ili kuhakikisha unapata wateja licha ya kuwa na ushindani. Pia unaweza kuuza bidhaa kwa bei ndogo ili kuwavutia wateja wengi zaidi. Jambo la msingi ni kuhakikisha unafanya maamuzi sahihi.

Weka bei kulingana na thamani

Ni muhimu kulijua soko vizuri ili kuweka bei ya msingi. Kwa mfano kama unaweza kununua seti ya sahani kwa Shilingi 15,000 na kutokana na thamani ya seti hiyo kuwa kubwa na wateja wakaonyesha nia ya kukunua hadi kwa bei ya Sh. 40,000 basi una uwezo wa kuweka bei hiyo. Aidha, epuka kuweka bei ndogo kupita kiasi kwani hutopata faida na hii itapelekea kufunga biashara vilevile kuweka bei kubwa kuliko thamani iliyopo sokoni kutasababisha kukosa wateja.

Mabadiliko

Mara nyingi bei, gharama, wateja na washindani hubadilika katika biashara. Hii humlazimu mfanyabiashara naye kubadilisha bei ili kuendana na hali ya soko. Hivyo basi, ni muhimu kuzingatia mambo yote yanayoendelea, ikiwa ni pamoja na kuzungumza na wateja mara kwa mara ili kuhakikisha bei yako inaendana na hali ya kifedha ya wateja wako.

Ikiwa bei inaonekana juu sana, unashauriwa kupunguza gharama zako na kupunguza bei ipasavyo kwa sababu siku zote, wateja huvutiwa na bidhaa zenye thamani na zinazouzwa kwa bei nafuu. Hivyo pangilia bei kulingana na wateja unaowalenga lakini hakikisha bidhaa yako au huduma ina thamani nzuri ambayo itamhamasisha mteja kurudi tena kwa mara nyingine

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter