Home BIASHARA Misamiati maarufu ya Forex na maana zake

Misamiati maarufu ya Forex na maana zake

0 comment 102 views

Katika kila biashara huwa kunakuwa na lugha maalum ya mawasiliano baina ya mteja na muuzaji/mfanyabiashara hivyo hata katika biashara ya Forex kuna maneno ambayo hutumiwa baina ya wabashiri katika biashara hiyo ili waweze kuelewana.

Yafuatayo ni baadhi ya maneno ambayo mtu anatakiwa kujua ili hali anataka kufanya biashara hii:

PAIR

Pair humaanisha mbili, hivyo katika biashara ya Forex humaanisha fedha za pande mbili. Ili kuweza kufanya biashara hii lazima kuwe na ununuzi au uuzaji kati ya sarafu za nchi mbili tofauti, nikimaanisha kuwa katika chati kuna upande wa kulia na kushoto hivyo ili kuweza kufanya forex, lazima ununue sarafu kutoka upande wa kulia na kuuza upande wa kushoto au ukiamua kuuza ya upande wa kulia inakupaswa ununue ya kushoto. Kwa mfano USD/JPJ, EUR/USD n.k.

Wakati wa ku-pair, sarafu huwa zinafanya CROSS na kama sarafu hizo zina thamani kubwa basi pair hiyo inakuwa na kasi kubwa. Inaelezwa kuwa Dollar ya Marekani (USD) ndio sarafu ya kwanza yenye nguvu kubwa kutokana na kuwa na uchumi mkubwa, siasa inayoeleweka na maendeleo kwa ujumla. Sarafu nyingine zenye nguvu ni EUR, GBP, JPY na CAD. Sarafu ambazo hazina nguvu sana na kasi yake huwa ya kawaida ni AUD, NZD na ZAR.

Sarafu katika chati ya Forex huandikwa kwa kifupi hivyo ntataja sarafu zinazotumiwa sana ili iwe rahisi kujua unanunua fedha za nchi gani.

USD – United States Dollar (Hii ni sarafu ya Marekani)

GBP – Great Britain Pound (Hii ni Paundi ya Britain)

EUR – Euro (Inayotumika Ukanda wa Ulaya)

CAD – Canadian Dollar (Inatumika Canada)

JPY – Japanese Yen (Inatumika Japan)

ZAR – South African Rand (Hii inatumika Afrika Kusini, ni sarafu pekee ya Afrika iliyopo kwenye chati ya Forex)

NZD – New Zealand Dollar (Hutumiwa New Zealand)

AUD – Australian Dollar (Hutumiwa Australia)

BASE CURRENCY

Base currency ni sarafu ya kwanza/kushoto katika pair yako. Kwa mfano: USDEUR, USD ndio base currency. Kila unapotaka kununua au kuuza, utakuwa unafanya na hii base currency.

QUOTE CURRENCY

Quote currency ni sarafu ya pili/kulia katika pair yako. Kwa mfano: USDEUR, EUR ndio quote currency. Ukibonyeza sehemu ya kuuza pair unakuwa umenunua pair hii na ukibonyeza sehemu ya kununua unakuwa umeuza pair hii. Unatakiwa kujua kwamba hizi pair kwa ujumla huwa zinakuwa zimeshapangwa, hivyo mfanyabiashara huchagua tu pair anazotaka.

BULL/BUYERS

Bull au Buyers ni wanunuzi wa pair ambapo wakiwa wananunua pair huwa inaitwa buying au going long.  Unashauriwa kama unataka kupata faida kama mnunuzi unatakiwa kununua sarafu wakati zinauzwa bei ya chini ili baadae uweze kuziuza kwa faida. Buyers wakiwa wengi na bei hupanda, kitendo hicho kinaitwa Bullish. Bei ikiwa bullish, mfanyabiashara anashauriwa kununua sarafu husika.

BEARS/SELLERS

Hawa ni wauzaji wa pair. Kitendo cha kuuza pair kinaitwa selling au going short. Kama wauzaji ni wengi, basi bei hushuka na kama wauzaji ni wachache bei nayo hupanda. Kitendo cha bei kushuka kinaitwa Bearish. Bei ikiwa bearish, mfanyabiashara anashauriwa kuuza ili asipate hasara.

BID PRICE

Bid price kwa kawaida hupangwa na Broker. Inakaa upande wa kushoto, hii huwa ni bei ya kuuza pair.

ASK PRICE

Hii bei pia hupangwa na broker, hukaa upande wa kulia, hii huwa ni bei ya kununua pair.Bei hii huwa kubwa kuliko Bid Price.

SPREAD

Spread ni tofauti kati ya Bid price na Asking Price ya pair husika.

Kwa mfano kama umekuta pair zinasoma EUR/USD-1.3277/1.3270 basi spread itakuwa ni 1.3277-1.3270= 7.

PIP

Watu wengine huita points. Hii ni tofauti kati ya bei uliyoingilia sokoni na bei uliyouza sarafu yako. Kwa maana nyingine ni faida utakayopata baada ya kuuza spair yako. Kwa mfano ulivonunua sarafu ulinunua EURUSD kwa 1.3270 ukasubiri bei ipande ukauza kwa 1.3277. Pip yako inakuwa 0.0007.

*Sarafu zote zina decimali nne kasoro sarafu ya Japan ambayo ina decimali mbili.

BROKER

Hutu ni mtu anayewaunganisha sellers na buyers kutoka duniani kote. Inaweza kuwa kampuni, au taasisi inayojishughulisha na mambo hayo. Wafanyabiashara humlipa kiasi fulani ili kuweza kufanya biashara hiyo.

LOT

Biashara ya forex hufanywa kwa lotsizes ambazo zimegawanywa katika makundi matatu ambayo ni Standard lot size (hii huwa na vipande vya sarafu husika 100,000) ya pili ni Mini lot (hii huwa na vipande 10,000 vya sarafu husika) na Micro lot (hii huwa na vipande 1000). Mfano ukinunua standard lot ya EURUSD kwa 1.3125 unakuwa umenunua Euro 100,000 na kuuza Dola 131,250.

LEVERAGE & MARGIN

Leverage ni kiasi cha fedha ambazo mfanyabiashara hupewa ili kufanya trade kulingana na size ya akaunti yake. Kwa mfano kama akaunti yako ina Dola 10,000.00 halafu Broker wako akakupa leverage ya 1:50, hii humaanisha kwamba utaweza kufanya biashara kwa limit ya 500,000 tu na si zaidi. Ili kufanya forex ya Dola 500,000.00, Broker atahitaji uweke asilimia kadhaa kwenye akaunti yako ndio uweze kununua au kuuza kwa mfano asilimia 2 ya dola 500,000.00. Hizo asilimia hufahamika kitaalamu kama Margin.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter