Home BIASHARA Mitandao ya kijamii inaua maduka ya kawaida?

Mitandao ya kijamii inaua maduka ya kawaida?

0 comment 185 views

Utandawazi umepelekea mabadiliko mbalimbali katika sekta ya biashara hapa nchini na duniani kwa ujumla. Uwepo ya mitandao umefanya hali wa wafanyabiashara walio na maduka kuwa ngumu kidogo kwani kutokana na urahisi wa kufanya manunuzi mitandaoni, watu wengi wanakosa sababu ya kwenda madukani. Uwepo na mitandao umeendelea kuwa tishio kwa wafanyabiashara ambao hapo awali walikuwa na uhakika wa wateja kwani watu walikuwa wakifika madukani kwao kwa ajili ya mahitaji yao ya kila siku.

Hivi sasa hali imebadilika kutokana na ukweli kwamba, kama unaweza kufanya kila kitu kupitia simu yako, kuna sababu gani ya kutoka nyumbani mpaka Kariakoo kufuata bidhaa wakati unaweza kuendelea na shuguli nyingine nyumbani na kuletewa mzigo wako moja kwa moja tena ndani ya muda mfupi tu?

Kwa mtazamo huo basi, unafikiri maduka ya kawaida yasiyotumia nguvu za mitandao ya kijamii yana hali gani? Je, imekuwa ngumu kwao kuwa na wateja wa uhakika kutokana na ushindani mkubwa ambao umetokana na biashara za mitandaoni? Kama mteja, ni gani unapendelea kufanya manunuzi yako? Je, unaenda moja kwa moja dukani au kila unachohitaji kinapatikana kwenye simu yako ya mkononi?

Maduka yanaweza kufanya yafuatayo ili kuhakikisha kuwa hayapo nyuma kwenye ushindani huu mkubwa.

Huduma bora kwa wateja – Kushawishi wateja kufika dukani moja kwa moja wakati wanaweza kupata mahitaji yao yote mtandaoni ni changamoto kubwa. Kama mmiliki wa duka, unaweza kuwa mbunifu kwa kuhakikisha kuwa wateja wanaofika dukani kwako wanapata huduma bora zaidi. Hakua mteja asiyeshawishika na huduma bora na ni vigumu kufanya hivi kwa njia ya mtandao. Hivyo tumia fursa hiyo kuhakikisha wateja wako wanapata huduma nzuri wanapotembelea duka lako. Kwa mfano, unaweza kuwasalimia kabla na baada ya manunuzi, unaweza kuwapa ushauri na kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi. Pia unaweza kuwa na ofa kama kutoa t-shirt kila baada ya kipindi fulani.

Kuwa sehemu ya jamii inayokuzunguka – Sifa kubwa ya biashara ya mitandaoni ni urahisi wa kupata huduma. Ikiwa una duka, wewe na biashara yako ni sehemu ya jamii. Hii inakuwa nafasi nzuri ya sio tu kuwa biashara ambayo watu hununua na kuondoka bali unakuwa ni sehemu ya maisha ya wanaokuzunguka. Tumia nafasi hiyo vizuri kwani jamii ndiyo wateja wako. Unapoishi vizuri na jamii unakuwa na uhakika wa kupata wateja wa kudumu.

Kubali mabadiliko – Kuna maelfu wa wafanyabiashara mitandaoni hivyo kuna sababu ya wafanyabiashara wa kawaida kuhakikisha kuwa hawabaki nyuma, Njia mojawapo ya kuendana na kasi hii ni kufanya mabadiliko mara kwa mara ili kwenda sambamba na muelekeo wa soko. Biashara zinazopingana na mabadiliko zinapata wakati mgumu kuendelea. Wafanyabiashara wanapaswa kuendana na mabadiliko yanayotokea katika soko.

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter