Home BIASHARA Nyama ya Mbuzi ya Tanzania yauzwa Qatar

Nyama ya Mbuzi ya Tanzania yauzwa Qatar

0 comment 233 views

Tani mbili za nyama ya Mbuzi zimesafirishwa jana January 23, 2022 kwenda Doha nchini Qatar.

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imesema wamefanikiwa kuwaunganisha wafanyabiashara wa ndani na masoko ya nje ya nchi ambapo kampuni ya Borema Affairs ndio wamesafirisha nyama iyo.

“Nyama hiyo ni sehemu ya mkataba wa kusafirisha Tani 120 sawa na Kilo 120,000 kwa kila mwezi kwenda Doha.
Fursa Hiyo inatokana na Mkataba wa kibiashara uliosainiwa kati ya Kampuni ya Borema Affairs na kampuni ya DLYLK for Food Trade iliyopo Doha- Qatar” TanTrade.
Mkataba huo ulisainiwa mnamo tarehe 22 Disemba, 2021 na ulishuhudiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi . Latifa Khamis.
Mkurugenzi wa Borema Affairs Bw.Thabit Mlangi ameishukuru TanTrade kwa kufanikiwa kumuunganisha na soko lenye uhakika huku akitoa wito kwa wafanyabiashara na wafugaji nchini kuendelea kuitumia Tantrade katika kutafuta masoko ya nje ya nchi .
Nae mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade ambaye ni Meneja wa Utafiti na Mipango Bw.John Fwalo ameipongeza Borema Affairs kwa kufanikisha mkataba huo kwa wakati na kutoa wito kwa wafanyabiashara nchini kutumia fursa zinazopatikana TanTrade ambazo ni za uhakika na zenye kufuata sheria na taratibu za nchi .
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade) pamoja na mambo mengine ina jukumu la kusimamia, kuratibu na kuendeleza biashara za ndani na nje ya nchi .

Soma Zaidi:Tanzania yafungua soko la parachichi Afrika Kusini

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter