Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amekerwa na tabia ya watendaji kutengeneza urasimu na kuchelewesha uboreshaji wa mnada wa ng’ombe wa Pugu.
RC Makalla amefanya ziara ya kushtukiza katika mnada huo baada ya kupata taarifa za malalamiko ya wananchi kutaka serikali iingilie kati uboreshaji wa mnada ikiwemo ujenzi wa uzio, sakafu, eneo salama la kupakilia ng’ombe, vyoo na kero ya ukosefu wa maji.
Baada ya ziara hiyo, Makalla ameagiza kuondolewa mara moja kwa tofali mbovu zilizoletwa kwenye eneo hilo kwaajili ya ujenzi wa ukuta baada ya kubaini tofali hizo hazina ubora.
Hata hivyo ameelekeza endapo mkandarasi hana uwezo wa kufanya maboeresho ya ujenzi katika eneo hilo yafanywe kwa kutumia Force akaunti.