Home BIASHARA Sababu 3 za kutumia Facebook kujitangaza

Sababu 3 za kutumia Facebook kujitangaza

0 comment 113 views

Kwa wafanyabiashara wengi siku hizi, mitandao ya kijamii imekuwa sehemu kubwa ya masiaha yao na hata mafanikio yake kutokana na kwamba, ni rahisi zaidi kuwafikia wateja wa aina mbalimbali kwa gharama nafuu. Mitandao ya kijamii ya Facebook na Instagram ndio inatumika zaidi na wajasiriamali wadogo hata wakubwa duniani kote kutokana na idadi kubwa ya watumiaji.

Wakati mwingine, sio lazima kutumia nguvu kubwa kujitangaza katika mitandao mingi kwa wakati mmoja na badala yake unaweza kuwekeza nguvu na fedha katika mtandao mmoja pekee na kupata matokeo mazuri. Facebook ni mtandao mzuri kwa ajili ya kutangaza biashara kwa sababu mbalimbali. Hizi hapa ni sababu kuu tatu kwanini kila mfanyabiashara anatakiwa kujitangaza katika mtandao huu.

Mtandao wa Facebook una watumiaji wengi zaidi kuliko mtandao wowote ule wa kijamii duniani kote. Kupitia mtandao huu ni rahisi zaidi kufikia wateja unaowalenga moja kwa moja tofauti na ilivyo katika mitandao mengine. Facebook inakadiriwa kuwa na watumiaji takribani milioni 2.41 kwa mwezi na kwa mujibu wa takwimu, asilimia kubwa zaidi ya watumiaji wa mtandao huu wana umri kati ya miaka 25-34.

Sababu nyingine ya kutumia mtandao huu kutangaza biashara yako ni kwamba, mtandao wa Facebook unamiliki mitandao mingine ya kijamii (Instagram, Facebook Messenger na Whatsapp) hivyo  inakupa urahisi kuunganisha watu wengi kwa wakati mmoja. Kwa mfano, unapotumia Instagram unaweza kualika marafiki zako wengine kutoka Facebook na hii hutengeneza mtandao mkubwa wa wateja.

Aidha, Facebook inafaa zaidi kwa wafanyabiashara kwa sababu inatoa nafasi ya matangazo (Facebook Ads) ambayo yanajitokeza upande mmoja wa ukurasa wako. Muundo huu wa matangazo unaonekana kuwa bora zaidi katika kutafuta masoko kwani tangazo linaweza kuwafikia watu wengi kwa urahisi na haraka.

Unapotumia mitandao/mtandao sahihi kujitangaza, ni wazi kuwa unawafikia wateja kwa urahisi zaidi na kuwa katika nafasi nzuri ya kukuza biashara yako. Kama bado hujaanza kutumia Facebook kwa ajili ya biashara yako, ni wakati wa kufanya mabadiliko ili kuwafikia watu wengi zaidi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter