Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage amesema maonyesho ya 42 ya kimataifa ya wafanyabiashara maarufu kama Sabasaba yamekidhi viwango vya DITF kutokana na kuwashirikisha wafanyabiashara wazawa pamoja na wale wa kimataifa. Mwijage amesema hayo wakati akimkaribisha mgeni rasmi katika maonyesho ya mwaka huu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutoa hotuba yake. Waziri Mwijage ameeleza kuwa, Sabasaba ya mwaka huu imehudhuriwa na takribani wafanyabiashara 2,900 wa ndani na wengine 2,500 kutoka nchi 33 za nje.
Kwa mujibu wa maelezo ya Waziri Mwijage, maonyesho ya Sabasaba ya mwaka huu yamekidhi viwango vya Maonyesho ya Kimataifa ya Wafanyabiashara (DITF) na washiriki wa maonyesho hayo wamefanikiwa kuonyesha bidhaa mbalimbali ambazo zimetengezwa na viwanda vya hapa kwetu.