Home BIASHARA Smartphone 5 kubwa za bei nafuu

Smartphone 5 kubwa za bei nafuu

0 comment 255 views

Simu mpya zinaendelea kutoka kadri siku zinavyoenda na ni wazi kuwa soko la bidhaa hili ni kubwa. Kila mtu anatamani kumiliki simu nzuri lakini wakati mwingine, gharama kubwa inakuwa kikwazo katika kufanikisha hilo. Ikiwa una bajeti ndogo, simu hizi tano ni kwa ajili yako kwani gharama zake ni nafuu kabisa.

Infinix Hot 6x

Simu hii inayopatikana kwa bei nafuu ya Sh. 320,000 ina betri kubwa (4000mAh) ambayo kulingana na matumizi, inaweza kudumu na chaji hadi kwa masaa 24.

Sifa zake:

Storage: 32 GB

RAM: 3/2 GB

Camera: 13 MP, 2 MP

Display: 6.2 inches.

Infinix Smart 3 Plus

Kwa bei ya Sh. 270,000 tu, simu janja hii inakuja na kamera tatu za nyuma pamoja na kioo kikubwa. Ikiwa unapenda sana kupiga picha, smart 3 plus ni kwa ajili yako.

Sifa zake:

Storage: 16-32 GB

RAM: 2/3 GB

Camera: Triple 13 MP, 2 MP, QVGA

Display: 6.2 inches.

Infinix Hot 7

Gharama ya simu hii sokoni ni Sh. 225,000. Ni smartphone yenye uwezo mkubwa kwa bei nafuu kabisa. Kma Infinix Smart 3 Plus hapo juu, Hot 7 ina kamera yenye uwezo wa kutoa picha za kuvutia. Pamoja na hayo, simu hii pia hukaa na chaji kwa muda mrefu.

Sifa zake:

Storage: 32 GB

RAM: ½ GB

Camera: 13 MP

Display: 6.2 inches

Samsung Galaxy A10

Simu hii bomba kabisa inapatikana dukani kwa bei nafuu ya Sh. 280,000 tu. Ukiachana na muundo wake wa kuvutia, Galaxy A10 ni moja kati ya simu za gharama nafuu zaidi kutoka Samsung.

Sifa zake:

Storage: 32 GB

RAM: 2 GB

Camera: 13 MP

Display: 6.2 inches.

Tecno Spark 3 Pro

Simu hii kutoka Tecno itakuwa ya kwanza kabisa kuwa na mfumo mpya wa Android 10 Q ambao bado upo katika hatua za majaribio hivi sasa. Ubora wake ni wa hali ya juu. Inapatikana na gharama ya Sh. 280,000 tu.

Sifa zake:

Storage: 32 GB

RAM: 2 GB

Camera: 13 MP, 2 MP

Display: 6.2 inches.

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter