Home BIASHARA TBS yaonywa bidhaa zisizo na viwango

TBS yaonywa bidhaa zisizo na viwango

0 comment 137 views

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Suleiman Murad Murad ametoa wito kwa Shirika la Viwango nchini (TBS) kushirikiana na Shirika la Viwango Zanzibar (ZBS) kuweka usimamizi katika mipaka ya Tanzania ili kuhakikisha bidhaa zisizo na viwango haziingii nchini na kuwadhuru watumiaji. Mwenyekiti huyo amesema hayo wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara katika shirika hilo na kujionea shughuli mbalimbali za udhibiti na ubora.

“Tunataka kuwe na usimamizi na ukaguzi katika mipaka na bandari zote na hata kwenye njia za panya kwa sababu kuwapo kwa bidhaa zisizokuwa na viwango kwenye soko kunawafanya muonekane hamfanyi kazi wakati mna mitambo ya kisasa”. Amesema Murad.

Pamoja na hayo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda amesema kuwa suala la uhaba wa wafanyakazi linashughulikiwa ili kuhakikisha shirika hilo linafanya kazi kwa uhakika huku akiagiza kutengenezwa kwa viwango vya madini ambavyo kwa sasa havipatikani nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dk. Yusuf Ngenya ametaja baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo kuwa ni pamoja na uhaba wa wafanyakazi, mishahara midogo, wafanyabiashara wasio waaminifu ambao huingiza biashara zao kwa njia ya panya, ufinyu wa nafasi maabara, gharama za kununua vifaa na vilevile wafanyabiashara kutopandishwa madaraja tangu mwaka 2016/17 ili kuwahamasisha katika kazi zao.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter