Na Mwandishi wetu
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Geoffrey Mwambe amewaambia waandishi wa habari kwamba kituo hicho kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na wafanyabiashara wenye viwanda nchini India wameandaa kongamano maalum ili kuhamasisha na kukuza uwekezaji nchini.
Kongamaano hili litafanyika Agosti 30 huko India na wawekezaji wa kampuni kubwa zaidi ya 100 watahudhuria na kampuni hizo zitasaidia kuitangazaTanzania.
Mwambe amesema lengo kubwa la kongamano hili ni kutangaza fursa za biashara pamoja na uwekezaji zilizopo hapa nchini. Uwekezaji huo utahusisha sekta mbalimbali kama vile viwanda, kilimo, afya, teknolojia ya habari na mawasiliano na nyinginezo.
Kampuni za kitanzania na sekta binafsi wanakaribishwa kushiriki kongamano hili ili kuendeleza ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji baina ya kampuni zetu na zile na nchi ya India.