Home FEDHA Vodacom yaingia rasmi DSE

Vodacom yaingia rasmi DSE

0 comment 70 views
Na Mwandishi wetu

Kampuni ya huduma za simu ya Vodacom imeorodheshwa rasmi kwenye Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE) jana Agosti 14 na imeweka sokoni jumla ya hisa zake bilioni 2.2. uzinduzi huo ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wa soko la hisa akiwemo Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.

Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Ian Ferrao amesema hatua hiyo ambayo ni maagizo ya serikali haikuja kirahisi, lakini walipata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wadau mbalimbali hadi kufanikisha jambo hilo.

Waziri wa Fedha ambaye alikua mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika katika ofisi za DSE ametoa pongezi kwa Vodacom na kuzitaka kampuni nyingine kuharakisha mchakato huu kabla hawajachukuliwa hatua za kisheria.

Mpango amesisitiza kuwa serikali itachukua hatua za kisheria kwa kampuni ambazo hazitatekeleza agizo hilo, pia amechukua nafasi hiyo kukumbusha kampuni hizo kushirikiana na wataalamu ya tasnia ya soko na mitaji kama Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA)  inavyoelekeza.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter