Home BIASHARA Tumia ubunifu kukuza biashara

Tumia ubunifu kukuza biashara

0 comment 100 views

Kadri siku zinavyozidi kwenda mbele ndivyo dunia inavyozidi kupanuka hasa katika suala zima la teknolojia. Ni ukweli usiopingika kuwa teknolojia imeweza kurahisisha utendaji kazi na uharaka wa utoaji huduma katika sehemu mbalimbali ulimwenguni.

Hii inatokana na ugunduzi unaoendana na ubunifu unaofanywa na wataalamu mbalimbali waliobobea aktika masuala ya sayansi na teknolojia, si wasomi tu bali kuna vitu mbalimbali vya kiubunifu na vya kipekee ambavyo vimefanywa na watu ambao sio wasomi bali wengine na kutokana na hali ya mazingira aliyopo na hivyo kuamua kutafuta njia mbadala itakayomfanya kuendana na uhalisia wa mazingira aliyopo.

Suala la ugunduzi na ubunifu limekuwa likijitokeza katika nyanja mbalimbali ikiwemo siasa, uchumi na kiutamaduni pia. Unapozungumzia katika uchumi kuna ugunduzi wa mashine za uzalishaji, uzalushaji bora na wa kitaalamu wa malighafi, kurahisisha huduma za usafiri na usafirishaji na mengineyo mengi.

Leo tutaangalia jinsi mfanyabiashara anavyoweza kutafuta njia mpya za kiubunifu ili kukuza biashara yake na kuifanya kuwa ya tofauti ukilinganisha na za wengine.

Kutokana na uhalisia wa kuwepo kwa ushindani wa soko katika masuala ya biashara, binadamu amekuwa akija na mbinu tofauti tofauti ili kuweza kutimiza

Kuelewa fasili na maana ya ubunifu

Kuna watu wanashindwa kutofautisha kati ya ubunifu na ugunduzi, Ugunduzi ni wazo jipya kabisa wakati Ubunifu ni kitendo cha kuja na mawazo mapya ya uboreshaji wa huduma au bidhaa iliyokuwepo toka awali kwa lengo la kuifanya yenye kufanikiwa zaidi. Hii inaweza kuwa kwa;

  • Kuboresha au kubadilisha uendeshaji wa biashara kwa kuongeza ufanisi wa uzalishaji au kuongeza ubora kwa bidhaa au huduma iliyokuwepo tangu awali
  • Kuendeleza au kutengeneza bidhaa au huduma mpya ili kuendana na uhitaji wa watumiaji
  • Kuiongezea thamani huduma au bidhaa yako ili ilete ushindani katika soko.

Ubunifu unaweza kufasiliwa kama ufunguaji wa huduma mpya au bidhaa ambayo haikuwepo mwanzo au kuwa kama mwendelezo wa mchakato kutoka bidhaa ndogo hadi kubwa. Ubunifu huu unaweza kufanyika ndani ya biashara kupitia wafanyakazi, meneja au nje ya biashara kupitia wsambazaji wa huduma au bidhaa, waandishi wa habari,wateja,watafiti wa masoko.

Kuwa na mbinu za ubunifu. Siku zote mfanyabiashara au mjasiriamali anapotaka kubuni  mbinu mpya au kuboresha ana lengo la kuipeleka biashara yake mbele zaidi. Hivyo ni vyema kusoma mazingira ya soko lako na uhitaji wa watu hao kwa sababu yote yanafanyika ili kuongeza thamani kwa wateja kwa mfano umeaffnaya utafiti na kugundua wateja wako wengi hawawezi kuzifikia bidhaa zako kwa urahisi katika soko unaweza kutafuta njia mbadala kwa kuwapelekea majumbani kwao.

Mipango juu ya ubunifu wako. Siku zote unapotaka kufanya maboresho ya huduma au bidhaa katika biashara yako tayari una malengo ambayo umepanga kuyafikia kupitia mchakato huo. Hivyo ni lazima kuna maeneo ambayo umedhamiria haswa kuyafikia kupitia ubunifu huo kwa sababu ubunifu hauifanyi tu biashara yako kukua bali unakuongezea faida.

Soma ushindani wa soko, tengeneza uhusiano mzuri na wateja wako,washirikishe washirika wa biashara yako na wasambazaji juu ya ubunifu ulioufanya kwenye biashara yako. Kisha unaweza kutafuta namna ya kujitathmini kutokana na maoni yao kama vile kujua endapo wafanyakazi wanauelewa wa kutosha, rasilimali kama zipo za kutosha

Ongeza hamasa. Wateja, wasambazaji wa huduma au bidhaa yako wana mchango mkubwa katika kuhamasisha juu ya ubunifu wa biashara yako, hivyo ni vema kuwapa muda wa kutoa maoni yao juu ya mabadiliko au maboresho ya baishara yako. Yapo mambo kadhaa unayoweza kufanya ili kuhamasisha ubunifu wa biashara yako. Utoaji wa ofa na zawadi kwa wateja ili waweze kukutambulisha sehemu nyingine,kuhamasisha uwasilishaji wa mawazo kuanzia mtu mmoja hadi kundi, kuwa na taswira ya kuajiri watu wenye ubunifu tofauti.

Wekeza katika ubunifu wako. Biashara yoyote ili iweze kukua inahitaji mfuko wa uendeshaji. Hivyo basi mfanyabiashara anashauriwa kuomba mkopo kutoka taasisi mbalimbali zinazohusika na utojai wa fedha endapo hata kuwa na fedha ya kutosha kuwez kuendesha biashara yake. Hii ni kutokana na ukweli kwamba biashara yoyote inahitaji mtaji na ubunifu huwa unaeda sambamba na upanuzi wa biashara kwa maana ya eneo pamoja na uzalishaji kuongezeka. Pesa atakayokopeshwa mfanyabiashara itamuwezesha kuweza kuitangaza biashara yake kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na runinga, radio na matangazo na gharamaza nyingineo ikiwemo usafirishaji.

 

 

 

 

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter