Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Unaifahamu vizuri biashara ya ubadilishaji fedha?

Unaifahamu vizuri biashara ya ubadilishaji fedha?

0 comment 29 views

Ubadilishaji fedha ni biashara ambayo imekuwepo kwa muda mrefu hata kabla ya uhuru. Biashara ya ubadilishaji fedha ni biashara imekuwa ikiwarahisishia kazi wageni wanaokuja nchini pamoja na watanzania wanaosafiri kwenda nje. Biashara ya ubadilishaji fedha inahusisha mabadilishano ya fedha za kigeni na zile za ndani kwa makubaliano yenye kwenda sambamba na thamani ya fedha kwa kila mmoja wapo.

Hii ni biashara ambayo kampuni kubwa za kifedha zimekuwa zikifanya ikiwemo Western Union na Paypal.

Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha una mipango madhubuti juu ya biashara yako ikiwa ni pamoja na kuwa na eneo la biashara lenye vitu vichache ikiwemo kompyuta, chumba cha kubadilishia fedha na huduma ya mtandao.

Kariakoo jijini Dar es salaam ni moja kati ya sehemu iliyojizolea umaarufu kutokana na biashara hiyo, lakini si Dar es salaam tu, bali sehemu nyingi hapa Tanzania zimekuwa pia zikifanya biashara hii. Zifuatazo ni njia za namna unavyoweza kuanzisha biashara ya ubadilishaji fedha na kufanikiwa ndani ya muda mfupi.

Zingatia eneo la biashara

Moja ya vitu vinavyofanya Kariakoo kuwa sehemu bora zaidi kwa ubadilishaji fedha ni kutokana na msongamano na uwingi wa fursa za biashara katika eneo hilo. Mtu yeyote anayetegemea kuanzisha biashara hii anashauriwa kuifanya katika sehemu yenye mkusanyiko wa watu na fursa nyingi za kibiashara.

Kibali na leseni ya biashara

Moja ya vitu vitakavyoifanya biashara yako kutambulika ni pamoja na kisajili sambamba na kutoa kodi. Serikali kupitia TRA imekuwa ikifuatilia kwa ukaribu kuhusu mwenendo wa ulipaji kodi, mapato na usajili wa biashara ili kuongeza mapato ya ndani. Kwa wale ambao wamekuwa wakikiuka biashara hizi mara nyingi biashara zao zimekuwa zikifungwa. Hivyo kufungua biashara bila kuwa na leseni ni kosa kubwa kisheria

Kufungua akaunti ya benki

Wafanyabiashara wa huduma za ubadilishaji fedha wanashauriwa kufungua akaunti za benki ili kurahisisha huduma na kufanya miamala popote walipo pasipo kujali muda au eneo.

Kutoa taarifa ya kodi na utunzaji kumbukumbu

Waswahili wanasema mali bila daftari huisha bila habari hivyo ni vizuri kuwa na kumbukumbu ya kile kinachofanyika ili kuepuka hasara hapo baadae.Lakini pia kutunza kumbukumbu za kodi ili TRA itakapouliza historia yako ya ulipaji kodi wa taasisi hiyo iwe rahisi kudhihirisha ubora wao katika ulipaji kodi.

Kuelewa mzunguko wa biashara

Mzunguko wa biashara ni kitu cha muhimu kufanya kwa sababu kupitia hilo itasaidia kujua namna ya kukabiliana.na ushindani wa watu wengine wenye biashara kama yako. Siku zote wateja wako wakigundua kuwa umekuwa ukitumia kima cha kuridhisha pindi unapobadilisha fedha watajaribu hata kuchukua akiba iliyobaki ili wamalizie.

Kama zilivyo biashara nyingine uthubutu na kuweka nia katika biashara yako, hivi vitu vinaweza kupima na kutabiri maisha yako ya baadae. Fursa hii ni kubwa wala haihitaji pesa nyingi sana badala yake Tanzania inahitaji mtu aliye tayari kufanya kazi na mwenye kujituma.

 

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter