Home BIASHARA UDBS bega kwa bega na wafanyabiashara nchini

UDBS bega kwa bega na wafanyabiashara nchini

0 comment 128 views
Na Mwandishi wetu

Mkuu wa Shule ya Biashara  ya Chuo Kikuu Cha Dar es salaam (UDBS), Dk. Ulingeta Mbamba amesema mkutano wa wajasiriamali, wadau na wataalamu wa biashara ulioanza jana alhamisi na kumalizika leo hii unadhamiria kujadili namna za kukuza biashara kwa kukutanisha wafanyabiashara ili kuimarisha biashara zao na hivyo kukuza pato la taifa.

Akifungua mkutano huo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Prof. Rwekeza Mukandala alisema kukutana kwa wadau hao wa biashara ni mbinu mojawapo ya wafanyabiashara wakubwa, wadogo na wa kati kujadili jitihada mojawapo ya kujenga uchumi wa taifa letu.

Mkutano huu unalenga kuwasaidia wajasiriamali na wafanyabiashara kupata mbinu za kufanikiwa kwani kuna changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo kama  mitaji midogo na mazingira kutokuwa rafiki kwao. Baada ya mkutano huu kukamilika, maazimio yatakayopatikana yatasambazwa kwa vyombo vya habari kusudi walengwa wengi zaidi wafahamu.

Dk. Mbamba ameongeza kuwa mada zaidi ya 50 zimewasilishwa kutoka ndani na nje ya nchi na kwamba UDBS itaendelea kuwa bega kwa bega na wafanyabiashara na kuwasaidia kutafuta mbinu mbadala ili kukuza masoko yao na pia kutunza fedha zao.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter