Home BIASHARA Umefikiria haya kabla ya kuwekeza katika biashara?

Umefikiria haya kabla ya kuwekeza katika biashara?

0 comment 336 views

Uwekezaji katika biashara ni moja kati ya nguzo kubwa zinazowapatia watanzania wengi kipato. Wengi wamekuwa na shauku ya kufanya biashara wakiamini ndio njia pekee itakayowapa mafanikio kwa urahisi. Sio uongo, japokuwa walio wengi hawafanikiwi kutokana na kutokuwa na mipango thabiti au mikakati ya kutosha katika uwekezaji huo. Kuna vitu ambavyo endapo utaamua kufanya biashara ni lazima vizingatiwe.

Vitu hivyo ni pamoja na:

  1. Punguza kuchanganya biashara na undugu/urafiki- Biashara inahitaji nidhamu kama zilivyo shughuli nyingine. Biashara ina sheria zake katika uendeshaji. Achana na yale mazoea ya kukopesha maana yatakurudisha nyuma kimaendeleo na biashara yako haitokua.
  2. Acha kuchanganya matumizi binafsi na yale ya biashara- Wengi hawaendelei na wanajikuta wamepata hasara mara baada ya kugundua pesa ya biashara ameipeleka kwenye matumizi yake ya kawaida kiasi cha kupelekea kushuka kwa mtaji.
  3. Punguza starehe- Starehe inahitaji pesa na inatumia pesa nyingi. Kama umeamua kuwa mjasiriamali/biashara jaribu kupunguza starehe na kuwa na nidhamu na fedha.

Mambo ambayo ukiyazingatia yatasaidia kukuza biashara yako ni haya yafuatayo:

  1. Soko. Soko kwa maana ya wanunuzi au wapokeaji wa huduma yako. Hakikisha kuwa upo sehemu sahihi na ina uhitaji wa bidhaa yako.  Pia Soko inaweza kutafsiriwa kwa maana ya utoaji wa huduma au uuzaji wa bidhaa kulingana na msimu. Mfano kama ni kipindi cha kombe la dunia ni dhahiri kuwa kutakuwa na manunuzi mengi ya jezi za mpira.
  2. Zingatia lugha. Ni vizuri kuonyesha ukarimu ili kumshawishi mteja arudi tena kufuata huduma siku nyingine.
  3. Jitofautishe na wengine- Unaweza  kuwa unatoa huduma inayofanana na watu wengine lakini watu wanapenda sana kuja kununua bidhaa au huduma kwako. Unaweza kujitofautisha na wengine kwa kutoa ofa, hali itakayo wafanya wateja wako kufurahia huduma yako na kujiona wao pia ni sehemu ya biashara yako
  4. Kujali muda- Kujali muda ni jambo muhimu sana kwa mfanyabiashara yoyote. Ni muhimu kuzingatia muda wa utoaji huduma katika biashara yako kwani itasaidia wapokeaji huduma kujua na kutambua uthubutu wako katika biashara.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter