Home BIASHARA Unataka kuanzisha biashara mtandaoni? soma hii

Unataka kuanzisha biashara mtandaoni? soma hii

0 comment 117 views

Mtandao wa intaneti umerahisisha kwa kiasi kikubwa suala la ujasiriamali na biashara. Kwani siku hizi watu wengi wanatumia intaneti kufanya biashara hata kama hawana eneo maalum (kupunguza gharama) la biashara hizo. Wengi wao wamekuwa wakifanya biashara zao majumbani na kujipatia faida kama kawaida.

Licha ya urahisi huo, ieleweke kuwa katika kila jambo ni muhimu kuweka mipango madhubuti ili kujua wapi kwa kuanzia, mahali ulipofikia na kujua kama kuna matumaini ya kufikia malengo au maono ya jambo hilo. Hivyo hata katika biashara za mtandaoni mfanyabiashara anatakiwa kutengeneza mipango ambayo itamsaidia mwanzoni mwa uanzilishi wa biashara, wakati wa kuendesha biashara hiyo na hata wakati wa mafanikio.

Ikiwa unataka kuanzisha biashara mtandaoni na huna vitu vifuatavyo, basi tambua hauko tayari kuanzisha biashara hiyo;

Fedha

Sawa huhitaji fedha nyingi kuanzisha biashara mtandaoni. Lakini kama huna fedha kabisa na unategemea faida ya haraka kupitia biashara ya mtandaoni kutatua mahitaji yako basi hauko tayari kuanzisha biashara hiyo. Kwani katika biashara yoyote uvumilivu ni jambo la msingi kwasababu ndio kwanza umetambulisha biashara yako, watu wengi hawana uhakika kama wanunue bidhaa hizo au la. Hivyo kadri muda unavyokwenda ndio wateja nao huona utofauti wa biashara yako na nyingine na kuamua kukuungisha zaidi. Hivyo ikiwa huna fedha na unategemea faida ya haraka  ni vyema ukasubiri ikiwa ni pamoja na kutafuta fedha katika ajira za kawaida hadi pale utakapokuwa tayari kuanzisha biashara huku ukiweza kumudu mahitaji ya kawaida hadi pale biashara yako itakapoanza kuzaa matunda.

Unataka kupumzika 

Watu wengi hushindwa kufanya biashara mtandaoni kutokana na mawazo waliyojiwekea kuwa biashara ya mtandaoni ni rahisi na haihitaji muda mwingi kuifanya hivyo ni rahisi kupata muda wa kupumzika. Ieleweke kuwa biashara ya mtandaoni inahitaji muda, na umakini -hasa pale inapokuwa imeanza kama biashara zinazofanyika moja kwa moja-katika maeneo husika. hivyo ikiwa unalengo la kufanya biashara mtandaoni ili uweze kupata muda wa kupumzika basi hauko tayari kufanya biashara hiyo.

Huna mpango madhubuti wa kuwafikia wateja walengwa

Biashara nyingi za mtandaoni zimeishia njiani kutokana na wamiliki wa biashara hizo kutokuwa na mpango madhubuti wa kuwafikia wateja husika wa bidhaa au huduma husika. hivyo kama hujui au hujatengeneza mpango wenye uhalisia wa kuwafikia wateja husika basi hauko tayari.

Wafanyabiashara wanatakiwa kujua kuwa kila siku biashara mpya zinafunguliwa kwa lengo la kupiku biashara ambazo zipo tayari. Hivyo ni muhimu kujikumbusha malengo ya kuanzisha biashara hiyo ili kuweza kuongeza jitihada ili kuweza kuwafikia wateja uliowalenga kwa wingi na kuwahamasisha wanunue bidhaa au huduma yako na si kutoka kwa washindani wako.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter