Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Vijana washauriwa kuwa washiriki katika maendeleo ya taifa

Vijana washauriwa kuwa washiriki katika maendeleo ya taifa

0 comment 30 views

Vijana hapa nchini wameshauriwa kuwa washiriki katika mipango ya maendeleo ya taifa na kuacha kulalamika na kuinyooshea mikono serikali na jumuiya ya kimataifa kuhusu ajira. Wito huo umetolewa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Alvaro Rodriguez alipokuwa akizungumza katika jukwaa la vijana la AIESEC. Rodriguez ameongeza kuwa vijana wasitegemee kuajiriwa au kupatiwa kazi kirahisi katika kipindi hiki ambacho theluthi mbili ya watu nchini ni vijana.  

Ameeleza kuwa tatizo la ajira kwa sasa lipo nje ya uwezo wa serikali au wahisani hivyo kuna kila sababu ya vijana kuwa wabunifu na kufanya shughuli ambazo zitawaletea maendeleo yao binafsi na ya kitaifa kwa ujumla. Amewashauri vijana kuwa watekelezaji na sio tu wasikilizaji.

Kwa upande wake, Rais wa AIESEC Amani Shayo amesema dhumuni kubwa la jukwaa hilo ni kuwaunganisha vijana na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuangalia namna ambavyo vijana wanaweza kuyafanyia kazi malengo yaliyopo katika maeneo yao.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter