Home BIASHARAUWEKEZAJI Biteko awatoa hofu wawekezaji

Biteko awatoa hofu wawekezaji

0 comment 104 views

Waziri wa Madini, Doto Biteko amesema mabadiliko katika Sheria ya Madini ya mwaka 2017 hayalengi kuwakandamiza wawekezaji kutoka nje na badala yake, yanalenga kuwanufaisha wawekezaji na watanzania wote kwa ujumla. Biteko amesema hayo wakati wa kikao chake na Balozi wa Canada nchini Pamela O’Donnel, ambacho kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa, na Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Augustine Ollal.

Waziri Biteko amesema madini ni rasilimali inayokwisha, hivyo yanapochimbwa yanapaswa kuwaletea faida watanzania na hata yamnapokwisha, wananchi wapaswa kujivunia rasilimali hiyo kutokana na maendeleo yaliyoletwa kama barabara, shule na ujenzi wa vituo vya afya.

“Sheria ya awali ilikuwa hainufaishi taifa na watanzania ndio maana mabadiliko yanafanyika. Mabadiliko ni kitu kizuri, tunahitaji rafiki atakayesababisha mabadiliko kutokea hivyo hawana haja ya kuogopa, tunawakaribisha kuwekeza”. Amesema Biteko.

Balozi O’Donnel amesema lengo la kukutana na uongozi wa Wizara hiyo ni kuelewa mabadiliko mbalimbali yaliyotokea katika sekta ya madini ili kuwatoa hofu wawekezaji kutoka Canada. Pamoja na hayo, Balozi huyo pia amehoji kuhusu masuala mengine ikiwemo utawala wa kisheria, mikataba ya madini, kodi, tozo pamoja na upatikanaji wa vibali vya kufanya kazi nchini kwa wananchi kutoka Canada.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter