Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uwekezaji, Prof Kitila Mkumbo amewataka watanzania kuacha fikra kwamba uwekezaji unahitaji watu kutoka nje ya nchi pekee.
Amewataka watanzania kuacha uoga na kusisitiza ni lazima kuwe na uthubutu wa uwekezaji hata kwa mitaji midogo.
Prof Mkumbo amesema “tukizungumzia ewekezaji watu wengi wanaona kama jambo kubwa hivi, zito na linahitaji wageni, lakini sio hivyo. Uwekezaji ni hatua ya mtu yeyeto anayochukua yeye binafsi au kampuni kuweka mtaji wa kufanya biashara na hatimae kupata faida”.