Home BIASHARAUWEKEZAJI Faida kwa wawekezaji Mfuko wa Umoja yaongezeka 2023/2024

Faida kwa wawekezaji Mfuko wa Umoja yaongezeka 2023/2024

0 comment 8 views

Thamani ya Mfuko wa Umoja chini ya Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS imeongezeka kutoka Shilingi bilioni 320 kipindi cha mwaka wa fedha ulioishia June 2023 hadi kufikia Shilingi bilioni 360 June 2024.

Aidha, faida kwa wawekezaji ilikuwa kubwa ikilinganishwa na kigezo linganifu (performance benchmark) ambapo kwa mwaka 2024 ilikuwa 12.1 ikilinganishwa na asilimia 11.2 ya mwaka ulioishia Juni 2023.

Mwenyekiti wa Bodi ya UTT AMIS Prof. Faustin Rweshabura Kamuzora ameeleza hayo katika Mkutano Mkuu wa Kumi na Sita wa mfuko wa Umoja uliofanyika Novemba katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

“Hadi kufikia June 2024, mfuko ulikuwa na ukubwa wa Shilingi bilioni 360.0 ambapo umeongezeka kwa Shilingi bilioni 40.0 sawa na asilimia 12.5 ikilinganishwa na Sh. bilioni 31.1 mwaka 2023,” imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa imeeleza kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha ulioshia June 2023, utendaji wa mfuko wa Umoja uliendelea kuwa mzuri ambapo faida ya wawekezaji kwa mwaka ilikuwa kubwa kulinganisha na kigezo linganifu.

“Faida ya mwaka ilikuwa asilimia 11.2 ikilinganishwa na asilimia 7.6 ya kigezo linganifu ambapo katika kipindi cha mwaka wa fedha ulioshia Juni 2023, thamani ya mfuko iliongezeka kutoka Shilingi bilioni 289.0 Juni 2022 hadi Shilingi bilioni 320.0 June 2023.

Ongezeko la thamani ya Mfuko linatokana na Imani ya wawekezaji pamoja na kueleweka kwa elimu iliyotolewa kuhusu faida ya uwekezaji wa pamoja,” imesema taarifa ya Mfuko wa Umoja.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa kwa mwaka 2024, thamani ya kipande imeongezeka kutoka Shilingi 926.9 hadi kufikia Shilingi 1,039.3 sawa na ongezeko la Shilingi 112.4 ikilinganishwa na ongezeko la Sh. 93.3 mwaka 2023.

Taarifa ya mwangalizi wa mfuko iliyosainiwa na Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela imeeleza kwamba maslahi ya wenye vipande ndani ya mfuko huo yanalindwa na kuzingatiwa ipasavyo.

“Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024 benki ya CRDB kama mwangalizi wa mfuko tumeendeleza uangalizi na mwenendo wa shughuli za meneja wa mfuko, utekelezaji wake na kuangalia changamoto kwenye uwekezaji,” imeeleza taarifa ya Nsekela.

UTT AMIS ni taasisi ya kipekee ya umma iliyoanzishwa na serikali mwaka 2003 kwa malengo ya pamoja na mengine, kuanzisha mifuko ya uwekezaji wa pamoja na kuwajengea wananchi utamadunu wa kuweka akiba na kufanya uwekezaji kupitia umiliki wa hisa zinazogawiwa kwa kununua vipande.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter