Home BIASHARAUWEKEZAJI FAIDA NNE ZA KUTUMIA MABANDA YA KISASA KWA UFUGAJI

FAIDA NNE ZA KUTUMIA MABANDA YA KISASA KWA UFUGAJI

0 comment 200 views

Jambo moja la msingi katika ufugaji wa kuku ni mabanda ya kufugia na kutokana na ubora wake, mfugaji anaweza kupata mafanikio au hasara kwani kuku hukua na hutaga zaidi katika mazingira mazuri na salama. Siku hizi kuna mabanda ya kisasa yaliyo katika mfumo wa betri ambayo yanamrahisishia mfugaji kufuga katika hali ya usafi na salama. Wafugaji wengi ambao wanatumia mabanda hayo wamekuwa wakifurahia matokeo.

Bei zake hutegemea aina ya banda na kiasi cha kuku waliopo lakini  kwa makadirio mabanda mengi ya kuku ya kisasa ya mfumo wa betri huuzwa kati ya Sh. 450,000 (kwa ajili ya vifaranga), uwezo wake ukiwa vifaranga 400, na kwa kuku wakubwa (layers) huuzwa kwa Sh. 750,000 na uwezo wake ni kuku 96 katika banda moja.

Hizi ni faida  nne za kutumia mabanda ya kisasa katika ufugaji wa kuku hususani wa mayai:

Huokoa nafasi

Kwa wafugaji wa kuku ambao wana changamoto ya nafasi kwa ajili ya kufugia wanaweza kusuluhisha changamoto hiyo kwa kutumia mfumo wa kisasa wa mabanda ya kufugia, kwani katika mabanda hayo ya kisasa huwa kunakuwa na nafasi ambayo kuku wanaweza kufugwa katika mpangilio mzuri zaidi. Kwa mfano kuna mabanda ambayo yanaweza kufuga kuku 96, kuna mabanda ambayo hukaa kama gorofa ambayo huruhusu ufugaji wa kuku 128 hadi 300 hivyo mkulima anaweza kununua banda ambalo linakidhi kiasi cha kuku anaotaka kufuga bila kuwaza kuhusu nafasi.

Gharama

Mabanda ya kisasa yaliyo katika mfumo wa betri yamerahisisha kazi kwa asilimia kubwa hivyo hakuna haja ya kuajiri watu wengi kwa ajili ya kuangalia kuku. Kila kitu kimeshapangwa katika mfumo huo, ikiwa ni pamoja na mpangilio wa kuku wenyewe, sehemu maalum ya kulisha na kuwawekea maji, sehemu ya mayai kupita na sehemu ya mfugaji kuchukua mayai hayo. Kazi iliyopo ni kuwamiminia chakula na maji kupitia maeneo yaliyotengwa na kuhakikisha mayai na uchafu yanatolewa kila baada ya muda ili kuku waendelee kutaga katika mazingira safi na salama.

Hupunguza magonjwa

Kutokana na kila kuku kuwa na sehemu yake si rahisi kuambukizana magonjwa. Pia mfumo maalum wa kutolea kinyesi unagfanya iwe ngumu kwa kuku kufikia kinyesi chao na kupata maambukizi mbalimbali. Vilevile ni rahisi zaidi kutambua na kuchukua hatua kwa kuku wenye magonjwa kabla hawajasambaza kwa  kuku wengine.

Aidha, ni muhimu kwa wafugaji kupewa elimu zaidi kuhusu teknolojia za kisasa zinazohusiana na ufugaji ili kuweza kunufaika na ufugaji wao bila kutumia nguvu nyingi. Watanzania wengi wameendelea kuwekeza katika sekta hii ya ufugaji hivyo ni wakati muafaka kwa serikali na wadau mbalimbali kuwaunga mkono kwa kuwapa elimu sahihi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter