Wataalamu wa masuala ya uchumi na uwekezaji kutoka nchini Indonesia wametua visiwani Zanzibar huku ikiwa zimepita takribani siku nane tangu Rais Wa Zanzibar Dk, Ali Mohamed Shein kuitembelea nchi hiyo kikazi.
Soma Pia STL Group kuwekeza Zanzibar
Akizungumza visiwani humo Waziri wa Fedha na Mipango (Zanzibar) Dk. Khalid Salum Muhammed amesema ugeni huo umeleta matumaini makubwa hasa katika sekta za viwanda, usafiri, mafuta pamoja na utalii. Akizungumza na wageni hao ofisini kwake , Waziri Muhammed amesema kuwa, wageni hao watakuwepo visiwani humo kwa muda wa wiki moja wakijadili na kuweka makubaliano juu ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo
Soma Pia Wakulima wa viungo washauriwa kuongeza uzalishaji
Kwa upande wake, Kiongozi wa msafara wa wawekezaji hao, Daniel Simanjuntak ameushukuru uongozi wa Zanzibar kwa kukubali kuanzisha ushirikiano ambao kwa kiasi kikubwa utachangia katika kuleta maendeleo kati ya nchi hizo mbili..