Katika kukabiliana na Virusi vya CORONA Mahakama ya Tanzania inajipanga kuanza kutumia mfumo wa Teknolojia wa TEHAMA na watuhumiwa hawatolazimika kufika mahakamani.
Akizungumza jijini Mwanza Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma alisema “Mahakama ni Taasisi ya Umma ambayo inatakiwa kutkeleza, maelekezo na Tahadhari zinazotolewa na Serikali yetu kupitia wizara ya afya.
Hivyo basi wadau wa mahakama wakiwemo wafungwa, maabusu, mawakili, wanannchi na wadau mbalimbali, wameshauliwa kukubali mabadiliko yanayoanza kuonekana mahakamani.
100