Home BIASHARAUWEKEZAJI Mauzo kati ya Tanzania, Saudi Arabia yapo chini: Waziri Kitila

Mauzo kati ya Tanzania, Saudi Arabia yapo chini: Waziri Kitila

0 comment 17 views

Imeelezwa kuwa kiwango cha biashara (mauzo) kati ya Tanzania na Saudi Arabia kiko chini na kimekuwa kikiunufaisha upande mmoja wa Saudi Arabia, ambapo wakati mauzo ya nje ya Saudi Arabia nchini Tanzania yakifikia dola za marekani bilioni 52.3, Tanzania imeiuzia nchi hiyo bidhaa zenye thamani ya dola milioni 12.3 pekee.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo ameeleza hayo wakati akifungua Jukwaa la Biashara na Uwekezaji lililoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC na Kituo cha kuendeleza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), lililofanyika makao Makuu ya Chemba ya Wafanyabiashara yalipo Riyadh nchini Saudi Arabia.

Prof. Mkumbo, alisema kuwa licha ya ushirikiano na uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo kudumu kwa zaidi ya miaka 40, bado kiwango cha biashara (mauzo) kati ya Tanzania na Saudi Arabia kiko chini na kimekuwa kikiunufaisha upande mmoja wa Saudi Arabia.

Ameeleza kuwa “mauzo ya nje ya Saudi Arabia nchini Tanzania yakifikia dola za marekani bilioni 52.3, Tanzania imeiuzia nchi hiyo bidhaa zenye thamani ya dola milioni 12.3 pekee”.

Alitoa wito kwa kampuni za Saudi Arabia kwa kushirikiana na wenzao wa Tanzania, kuongeza uwekezaji na kiwango cha biashara kati ya nchi hizo mbili kwa kutumia fursa za kiuchumi na mazingira bora ya uwekezaji yaliyopo hivi sasa nchini Tanzania kuwekeza mitaji ili kunufaika na soko kubwa linalipatikana nchini Tanzania na nchi jirani.

Ametaja maeneo ya uwekezaji ikiwemo sekta za kilimo, usindikaji bidhaa za kilimo, nishati ya kijani, uchumi wa buluu, madini, mafuta na gesi pamoja na masuala ya kidigitali.

Jukwaa hilo limewaleta pamoja wafanyabiashara wa Tanzania na Saudi Arabia, ambapo kwa siku kadhaa, watapata nafasi ya kujadiliana kuhusu fursa za uwekezaji zinazopatikana katika nchi hizo mbili ili kukuza biashara na uwekezaji, hatua ambayo lengo lake ni kuinua na kukuza zaidi uchumi wa nchi hizo mbili.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter