Home BIASHARAUWEKEZAJI Sekta binafsi changamkieni fursa: Rais Samia

Sekta binafsi changamkieni fursa: Rais Samia

0 comment 85 views

Rais Samia Suluhu Hassan imeitaka Sekta Binafsi nchini kuchangamkia fursa ya kujenga hoteli kwa ajili ya watalii.

Rais Samia amesema hayo wakati akifungua na kushiriki Mkutano wa 14 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Ikulu, jijini Dar es Salaam.

“Wageni wanaokuja mwakani na mwaka unaofuata watakosa mahali pa kulala kama hatukuchangamka kwenye kujenga hoteli sasa hivi, sekta binafsi ni fursa muhimu” amesema Rais.

Amesema tafiti ndogo iliyofanyika inaonyesha kuwa wageni waliokuja mwaka jana ni asilimia 30 tuu wamerudi mwaka huu.

Amesema hii inaonesha kuwa Tanzania wageni wanakuja lakini hawataki kurudi pamoja na vivutio vilivyopo.

Ameitaka sekta ya utalii kuangalia kasoro zilizopo na kuzifanyia marekebisho ili wageni wawe wanarudi na kuwafanya wenzao kuja Tanzania.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter