Home BIASHARAUWEKEZAJI Sekta ya madini Tanzania inakuwa kwa asilimia 17

Sekta ya madini Tanzania inakuwa kwa asilimia 17

0 comment 126 views

Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan ameafungua Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika sekta ya Madini Tanzania ambapo amewataka wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali duniani kuwekeza katika sekta hiyo.

Amesema mwaka jana sekta ya madini iliongoza kwa ukuaji kwa 17.7% pamoja na uuzaji wa vito vya thamani kubwa nje ya nchi.

Katika hotuba yake amesema “niungane na wito wa kiongozi wetu Rais Magufuli kuwakaribisha wote mnaofuatilia kongamano hili kwa njia ya video na wote wenye nia ya kuwekeza katika sekta hii inayokuwa kwa kasi kubwa sana”.

Aidha, Makamu wa Rais amesema utungaji wa sheria kali ya kudhibiti madini ilikuwa na nia ya kuhakikisha rasilimali madini inamnufaisha mtanzania na kukuza pato la taifa katika sekta hiyo ambayo inategemea kuchangia pato la taifa kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2025.
Amesema vitendo vya wizi wa madini kwa miaka mingi kabla ya kuwepo kwa sheria za kudhibiti wizi huo madini mengi yalikuwa yanasafirishwa nje ya nchi bila taifa kunufaika na rasilimali hiyo kama ilivyo kwa sasa.
Ameongeza kuwa, pamoja na janga la Corona lililoleta changamoto ya uzalishaji na soko la uhakika, mwaka jana Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi tano barani Afrika ambazo ni wazalishaji wakubwa wa madini ya dhahabu.

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter