Home BIASHARAUWEKEZAJI Serikali yataka wawekezaji kufuata sheria

Serikali yataka wawekezaji kufuata sheria

0 comment 104 views

Serikali kupitia wizara ya Sera, Bunge Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu imewaondolea hofu wawekezaji na badala yake kuwataka kufuata sheria za nchi ili kuepuka usumbufu kutoka serikalini pindi wanapokiuka sheria.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Antony Mavunde katika mkutano ulioandaliwa na Chama cha Wafanyakazi na Wawekezaji kutoka nchini China kwa lengo la kuendelea kuimarisha mahusiano mazuri ya kibiashara.

Waziri Mavunde amesema kuwa amefurahishwa na mkutano huo ambao lengo kuu lilikuwa ni kuzungumzia sheria za kazi na vibali vya wakazi.

Soma Pia Wawekezaji dawa za mifugo washauriwa kuchangamkia fursa

Waziri Mavunde ameeleza kuwa serikali ya awamu ya tano inahitaji sana wawekezaji kwa ajili ya kuleta maendeleo nchini, sanjari na kuongeza fursa za ajira kwa vijana wa kitanzania.

“Serikali ya Tanzania inawahitaji sana wawekezaji wanaofuata sheria za kazi na ukaazi (uhamiaji) kwa Wafanyakazi na wataalamu watakaoletwa nchini”

Aidha Waziri  Mavunde amepongeza juhudi kubwa zilizofanywa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa kuweza kutafsiri sheria za kazi kutoka lugha ya kiswahili kwenda kichina ili kuwarahisishia wawekezaji hao kuzielewa vizuri sheria hizo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ATE Dk. Aggrey Mlimuka ameishukuru serikali kuitikia mwaliko, huku akisisitiza kuwa lengo la mwaliko huo ni kuikutanisha serikali na wawekezaji kujadili namna nzuri ya kukuza sekta ya uwekezaji kwa sababu uwekezaji mzuri ni ule unaoendana na mazingira mazuri sambamba na utii wa sheria zilizowekwa nchini.

Soma Pia Uboreshaji wa miundombinu wavutia wawekezaji

Akielezea baadhi ya changamoto wanazopata wawekezaji Dk. Mlimuka amesema ucheleweshaji wa vibali kwa mwekezaji, kutotii sheria za makazi hapa nchini ni baadhi ya vitu vinavyorudisha nyuma uwekezaji nchini.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter