Home BIASHARA ATCL kuimarika kufikia 2023

ATCL kuimarika kufikia 2023

0 comment 35 views

Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) linatarajia kuanza kupata faida mwaka 2023 kama hali ya biashara ikiendelea kama ilivyo hivi sasa. Shirika hilo linalomiliki ndege nne ikiwemo ya kisasa aina ya Boeing Dreamliner yenye uwezo wa kubeba abiria takribani 262 limekuwa likijiendesha kwa hasara japo hasara hiyo inazidi kushuka kila mwaka ambapo kwa mwaka 2016 hasara ilikuwa Sh. 14.4 bilioni na huku ikishuka hadi Sh.4.2 bilioni kwa mwaka 2017.

Haya yanakuja baada ya shirika hilo kuanzisha mpango biashara wa hadi mwaka 2022 ambapo kazi itakuwa ni kukuza mapato kwa kupunguza hasara za kizembe, ufisadi na kuboresha huduma kwa wateja ili kuwavutia zaidi.

Mbali na hayo, ATCL imejipanga kuongeza safari za ndani za nje ya nchi hasa nchi jirani kama Uganda na Burundi kuanzia mwezi huu na hadi kufikia mwishoni mwa mwaka, shirika litaanzisha safari za India na China. Shirika hilo pia limethibitisha kuanzisha safari za Ulaya baada ya kuwasili kwa ndege nyingine kubwa aina ya Dreamliner mwakani.

ATCL ni shirika la ndege la Tanzania ambalo baada ya kuyumba kibiashara kwa muda, limeimarishwa na serikali ya awamu ya tano kwa kununua ndege sita aina ya bombardier na boeing zilizoamsha upya biashara kwa shirika hilo huku baadhi ya ndege hizo zimewasili huku zingine zikitarajia kuwasili kwa awamu hadi kufikia mwaka 2020.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter