Home BIASHARAUWEKEZAJI Serikali yatumia bilioni 32 kupunguza umaskini

Serikali yatumia bilioni 32 kupunguza umaskini

0 comment 114 views

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Mkuchika amesema takribani Sh. 32 bilioni zimetumika kupunguza tatizo la umaskini kupitia Mpango wa Kupunguza Kaya Masikini (Tasaf) tangu mpango huo kuanza utekelezaji. Waziri huyo ameeleza Bunge kuwa Sh. 7, 240, 498, 800 zimetumika kwenye miradi ya kutoa ajira za muda huku Sh. 25.24 bilioni zikiwa ruzuku kwa ajili ya sekta za elimu na afya wakati Sh. 464 milioni zikitumika kwa ruzuku kwa vikundi vya kuinua uchumi wa kaya.

Waziri Mkuchika amewataarifu wabunge kuwa, mpango wa Tasaf unatekelezwa kwa awamu kwenye halmashauri zote bara na visiwani na utakamilika ifikapo mwaka 2020/2023. Hadi hivi sasa, jumla ya kaya milioni 1.1 zenye watu takribani milioni tano zimeandikishwa kwenye vijiji, mitaa na shehia 9,986 nchi nzima.

Kwa upande wa Zanzibar, Unguja na Pemba Mkuchika amesema kaya 32,262 kutoka shehia 168 zimenufaika na mpango huo akitaja kaya 18,092 ni kutoka Unguja na 14,164 zikitokea Pemba.

“Lakini pia nataka niwapongeze walengwa wa Tasaf Unguja na Pemba. Katika nchi yetu, mikoa inayoongoza kwa kufanya vizuri miradi ya Tasaf ni mikoa ya Unguja na Pemba. Na kwa maana hiyo, nataka nimpongeze Waziri mwenzangu Mohammed Aboud Mohammed anayesimamia Tasaf kule Pemba na Zanzibar ambaye anamsaidia Makamu wa Rais ambaye ndiye Waziri mwenye dhamana ya Tasaf Zanzibar”. Ameongea Mkuchika.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter