Home BIASHARAUWEKEZAJI Wabunge wataka Maliasili iongezewe bajeti

Wabunge wataka Maliasili iongezewe bajeti

0 comment 122 views

Wabunge wameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mapinduzi makubwa yanayofanywa hivi sasa na kutaka wizara hiyo iongezewe bajeti ili iweze kufanya vizuri zaidi katika mwaka wa fedha 2023/24.

Baadhi ya wabunge waliochangia hotuba ya Wizara ya Maliasili na Utalii, ni Mbunge wa viti maalum Njombe (CCM) Neema Mgaya ameitaka Serikali kuangalia namna ya kurudisha fukwe na visiwa vyote katika Wizara ya Maliasili na Utalii ili visimamiwe na Bodi ya Utalii nchini ili kuweza kuuza utalii wa nchi kwa pamoja kama inavyofanyika katika nchi nyingi duniani.

Aidha, amesema nchi kama Ushelisheli zimekuwa zikitegemea utalii wa fukwe na bahari pekee ambapo amefafanua kuwa Tanzania imebarikiwa kuwa na fukwe nzuri kuliko nchi nyingi duniani na endapo zitasimamiwa vizuri zitakuwa na mchango mkubwa kwenye uchumi.

Aidha, ameishauri pia serikali kuona umuhimu wa kujenga hoteli kwa ajili ya kuwalaza wageni ambao wameanza kumiminika kufuatia mikakati mizuri iliyowekwa na Wizara na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Filamu ya The Royal Tour.

Mbunge mwingine Benedetha Mshashu ameipongeza Wizara na Serikali kwa ujumla kwa mikakati ya kukuza na kutangaza utalii na amesema imezaa matunda ambapo ameomba Wizara kuviendeleza visiwa vidogo vidogo 48 vilivyopo katika mkoa wa Kagera ili viweze kuchangia kikamilifu kwenye uchumi.

Wabunge hao wameeleza hayo June 5, 2023 wakati wa kuchangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya mwaka 2023/24 iliyowasilishwa bungeni na Waziri wa Maliasili na Utalii Mohamed Mchengerwa June 2, 2023.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter