Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya usalama wilayani humo Jokate Mwegelo amewataka wawekezaji kufuata kanuni na sheria za uwekezaji zikiwemo ulipaji kodi bila shuruti kwa manufaa ya wawekezaji na taifa kwa ujumla.
Soma Pia Majaliwa akaribisha wawekezaji kutoka China
Mwegelo ameyasema hayo katika kikao cha serikali ya wilaya ya Kisarawe na Kamishna wa madini ukanda wa mashariki Mhandisi Ally Maganga baada ya kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika kampuni ya Rak Kaolin inayojishusisha na uchimbaji wa madini ya Kaolin na kukuta bado inaendelea na uchimbaji licha ya kuzuiwa na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo.
Soma Pia Bodi ya maziwa yakaribisha wawekezaji
Ukaguzi uliofanywa na Mwegelo pamoja na kamati ya madini ulifanikiwa kukamata malori matatu yaliyobeba tani 100 za madini hayo zenye thamani ya Sh. 2,100,000 za kitanzania, na kuamuru kampuni kulipa faini ya ukiukaji wa maagizo ya Naibu Waziri kwa kufuata Sheria ya Madini ya mwaka 2010 na marekebisho yake ya mwaka 2017. Mwegelo pia ameagiza kampuni hiyo kulipa kodi yote ambayo imekwepa.