Home BIASHARA Tanzania kushiriki maonyesho ya biashara China

Tanzania kushiriki maonyesho ya biashara China

0 comment 41 views

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Tanzania ipo mbioni kukamilisha taratibu za kuwa moja kati ya washiriki wa maonyesho ya biashara na uwekezaji nchini China. Katika maonyesho hayo yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni, banda la Tanzania ambayo ndio nchi pekee kutoka Afrika Mashariki kushiriki katika maonyesho hayo, litajumuisha wajasiriamali, wawekezaji pamoja na wafanyabiashara.

Akizungumza na Balozi mdogo wa China visiwani Zanzibar Xie Xiaolon, Balozi Iddi ameishukuru China kwa kuipatia Tanzania nafasi hiyo ya kipekee na kusisitiza kuwa, Tanzania na Zanzibar zinaichukulia nchi hiyo (China) kama rafiki wa kweli kutokana na kujitolea kwake katika maendeleo ya nchi pamoja na bara la Afrika kwa ujumla

Kwa upande wake, Balozi Xiaolon wa China amesema nchi yake imedhamiria kutoa fursa kwa Afrika kuimarika kiuchumi na kuongeza kuwa serikali ya China imeweka kipaumbele kwa bara la Afrika ili kusaidia kufufua uchumi. Katika maelezo yake, Balozi huyo amesema tayari tayari mpango umeonyesha mafanikio ikiwa ni pamoja na misaada ya kiuchumi ambayo inaenda sambamba na ongezeko la kampuni na taasisi za uwekezaji.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter