Home BIASHARAUWEKEZAJI Wawekezaji waendelea kuongezeka

Wawekezaji waendelea kuongezeka

0 comment 178 views

Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA) imesema kuwa maboresho yaliyofanywa na shirika hilo yameongeza idadi ya wawekezaji hapa nchini. Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji wa mamlaka hiyo, James Maziku amesema hayo wakati wa mkutano wa kibiashara na wawakilishi kutoka Hong Kong.

Maziku ametaja kati ya sekta zinazowavutia wawekezaji hao kuwekeza nchini ni pamoja na sekta ya kilimo na madini. Tafiti iliyofanywa na muonekano wa uchumi na fursa za uwekezaji Afrika imetaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazowavutia zaidi wawekezaji barani Afrika.

Akiiwakilisha Macau katika mkutano huo, Jessica So, amesema wamepata maelekezo kuhusu fursa za uwekezaji nchini Tanzania baada ya vikao na EPZA pamoja na TIC na hivyo hawatosita kurudi Tanzania kuwekeza.

“Fursa za uwekezaji nchini Tanzania zinahamasisha, tukirudi nyumbani tutafanya maamuzi ya kuja kuwekeza hasa katika sekta ya kilimo”. Amesema So.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter