Home BIASHARAUWEKEZAJI Waziri ahimiza uwekezaji sekta ya utalii

Waziri ahimiza uwekezaji sekta ya utalii

0 comment 156 views

Wizara ya Maliasili na Utalii imesema itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kutangaza vivutio vya utalii na fursa za uwekezaji zilizo katika sekta ya utalii ndani na nje ya nchi.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana amesema hayo alipokuwa akitoa salamu za Wizara wakati wa kufunga Maonesho ya Utalii Karibu Kusini mkoani Iringa.
Amesema Tanzania hususani mikoa ya Kusini ina maeneo mengi yenye vivutio vya Utalii ambayo ni vya kipekee duniani kama vile Hifadhi ya Taifa ya Ruaha yenye makundi makubwa ya Tembo na wanyamapori wengine, Hifadhi ya Taifa ya Kitulo yenye aina mbalimbali za maua, Utamaduni na vingine vingi.

“Tunahitaji wawekezaji wa maeneo mbalimbali, nchi imetulia tunakwenda tuna amani, ushirikiano haya yote yanachangia katika utalii na uwekezaji.

Tuna utalii wa mila na desturi, sasa tumeanza na utalii wa vyakula, watu waje watesti vyakula vya nyanda za juu Kusini,” amesema”.
Aidha Balozi Dkt Chana amemshukuru Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi Kwa kumtuma Makamu wake wa Kwanza wa Rais Mhe. Othman Masoud amwakilishe kufunga maonesho hayo ambayo ni moja ya zao la Utalii la mikoa ya Kusini.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter