Home BIASHARAUWEKEZAJI Zanzibar yaendelea kukuza utalii

Zanzibar yaendelea kukuza utalii

0 comment 106 views

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema malengo ya Mkutano wa Wadau wa Biashara ya Utalii (Z- Summit) unalenga kutangaza fursa na kukuza zaidi utalii wa Zanzibar.

Dk.Mwinyi amesema Serikali inajitahidi kuweka mazingira ya kuvutia zaidi ya Uwekezaji Zanzibar ili kuwa kivutio cha wawekezaji na watalii na kuepuka athari za mazingira kwenye rasilimali za visiwani.

“Sekta ya utalii duniani inachangia uchafuzi wa mazingira, upotevu wa viumbe hai, mabadiliko ya tabia ya nchi, hewa na maji hivyo tushikamane kuhakikisha Zanzibar ibaki na uhifadhi mzuri wa mazingira,” amesema Rais Mwinyi.

Rais Mwinyi amesema utalii unachangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa Zanzibar kwa karibu asilimia 30 hivyo Serikali imejitolea kukidhi mahitaji ya soko la utalii kwa kujipanga kwa kufikia idadi ya watalii 850,000 ifikapo mwaka 2025.

Rais Dk. Mwinyi amebainisha hayo wakati akizindua Mkutano wa Wadau wa Biashara ya Utalii (Z- Summit) katika Hoteli ya Golden Tulip Aiport Zanzibar.

Kabla ya kuzindua mkutano huo Rais Dk. Mwinyi alitembelea mabanda ya wadau mbalimbali wa Utalii kutoka ndani na nje ya nchi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter