Vikundi 37 vya jiji la Tanga vimepokea Sh. millioni 300 ikiwa ni mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri ya jiji.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Ummy Mwalimu amekabidhi hundi ya fedha hizo ambazo ni mapato ya ndani kwa kipindi cha robo tatu ya mwaka 2020/2021.
Waziri Ummy amesema “ni furaha kwangu kuona jiji mmetimiza wajibu sasa nivitake vikundi ambavyo mnapokea fedha hizi mkazifanyie kazi na kuzirejesha kwa wakati ili wenzenu wengine waweze kunufaika na mikopo hii.”
Daudi Maeje ambae ni Mkurugenzi wa jiji la Tanga amesema kwa bajeti ya jiji, walipanga kutoa mikopo ya asilimia 10 yenye jumla ya Sh bilioni 1.2 ambapo mpaka sasa wameshatoa Sh. million 994 sawa na 81% ya malengo.