Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi Vodacom Tanzania imejumuika na wafanyakazi wake kuuaga mwaka 2018. Sherehe hiyo ilifanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam ambapo pia kampuni hiyo iliwazawadia wafanyakazi wake bora.

Wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom Tanzania PLC, wakisakata muziki wakati wa sherehe ya kuuaga mwaka 2018 iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano, Rosalynn Mworia, (Kushoto) akimsikiliza Goodluck Mushi, wakati akishukuru kwa kutunukiwa tuzo ya mfanyakazi bora wakati wa sherehe ya kuuaga mwaka 2018 iliyofanyika Mlimani City Jijijini Dar es Salaam.