Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi Vodacom imeendelea kusogeza huduma zake karibu kwa wateja wake kwa kufungua duka jipya ‘Vodashop’ katika eneo la kwamrombo jijini Arusha.
Tukio la uzinduzi lilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo na Mkuu wa Mauzo ya Vodacom Kanda ya Kaskazini, Brigita Stephen pamoja na wafanyakazi wa Vodacom.

Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo (kulia) na Mkuu wa mauzo wa Vodacom Kanda ya Kaskazini, Brigita Stephen wakizindua duka la Vodacom litakalowahudumia wateja eneo la Kwamrombo jijini Arusha, wa tatu kushoto ni mdau wa Vodacom Bakari Fungo.

Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kushoto) akiwa pamoja na Mkuu wa mauzo wa Vodacom Kanda ya Kaskazini Brigita Stephen(kulia) wakati wa uzinduzi wa duka la Vodacom eneo la Kwamrombo jijini Arusha.

Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (katikati) akimsikiliza Mkuu Vodacom Kanda ya Kaskazini, Brigita Stephen (kushoto) wakati wa uzinduzi wa duka la Vodacom eneo la Kwamrombo jijini Arusha, kulia ni mdau wa Vodacom Bakari Fungo.