Home BIASHARA Biashara zaidi ya moja inawezekana

Biashara zaidi ya moja inawezekana

0 comment 46 views

Ipo mifano mingi tu ya wafanyabiashara na wajasiriamali amabo wamethubutu kwa namna moja au nyingine kuanzisha biashara zaidi ya moja na wakati mwingine hata tatu na bado baishara zao zimeendelea kuimarika. Mfano mzuri ni Said Salim Bakhresa, huyu ni mfanyabiashara mkubwa nchini ambaye ameweza kufanikiwa kwa kuwa na biashara tofauti tofauti na kubwa ambazo zimeendelea kuwepo hadi sasa na zinafanya kazi vizuri. Bakhresa anamiliki chombo cha habari cha Azam, pia anamiliki klabu ya Azam FC, kiwanda cha unga na vinywaji cha Azam, na miradi mingine mingi,.

Wewe ni nani hata ushindwe kufanikiwa kuwekeza katika miradi zaidi ya mmoja? Leo tutajikita katika kujifunza jinsi mjasirimali/mfanyabiashara anavyoweza kuwa na biashara zaidi ya moja na akafanikiwa. Baadhi ya masuala ya kuzingatia ili kufanikisha hilo ni hizi hapa chini:

  1. Kuwa na ujuzi. kwa kila biashara. Kuwa na ujuzi kwa kila biashara ni jambo ambalo litakusaidia kuzisimamia biashara hizi mbili. Hivyo lazima kuhakikisha kila biashara inafanyika kwa umakini mkubwa wenye kuendana sambamba na kuchukua maamuzi haraka katika kutekeleza mambo. Jitahidi kusoma vitabu kwa ajili ya kupata ujuzi zaidi sambamba na kujifunza ushindani katika soko kwa kila biashara na kama unaona hauna ujuzi juu ya kazi hiyo, ni vyema kuajiri mtu mwenye uelewa wa kutosha
  2. Mpangilio wa muda. Kupanga mambo yako kwa kufuata ratiba itakusaidia kufanya kila biashara kwa wakati wake kwa kufuata ratiba na muda uliojipangia kuifanya. Hii itasaidia katika kuondoa mkanganyiko wa biashara na muingiliano wa. Kama wewe una masaa 24 hata matajiri unaowaona leo duniani nao wana masaa 24 kama wewe lakini kinachokutofautisha nao ni namna ya utumiaji wa muda. Ukidhamiria na kila biashara ukaifuatilia kwa muda unaotakiwa basi biashara zako zote zitafanikiwa.
  3. Tafuta wasaidizi. Matajiri na wajasiriamali wengi hawajafanikiwa kuwa na biashara nyingi kwa kusimamia wao wenyewe bali kuna watu ambao wameajiriwa na wanafanya kazi kwa niaba ya wamiliki. Hivyo basi kuajiri wasaidizi katika bishara zao ni njia bora na salama itakayookoa biashara zako zisianguke na badala yake zizidi kustawi.
  4. Weka malengo na jaribu kuyatekeleza. Mfanyabiashara mwenye biashara zaidi ya moja lazima aishi kwa kufuata mipango aliyojiwekea kwa maana ya siku, wiki, mwezi na hata mwaka. Kuhakikisha yale yote aliyopanga kuyatekeleza kwa kila biashara yanafuatwa na kutekelezwa kama yalivyo kwenye kalenda ya mipango yake.
  5. Changanua biashara kwa kuzitenganisha. Huu ni mtihani mkubwa wanaopitia wafanyabiashara wengi kuhusianisha biashara moja na nyingine kwa maana ya mitaji, vifaa, matumizi, wafanyakazi na usimamizi. Ukifanya hivyo unakosea kwa sababu kila biashara inatakiwa kujitegemea na kuwa na usimamizi wake binafsi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter