Home BIASHARA Wachimbaji Chunya furaha tupu

Wachimbaji Chunya furaha tupu

0 comment 100 views

Wachimbaji wadogo wa dhahabu wilayani Chunya mkoani Mbeya wamefanya maandamano kufuatia maamuzi ya Rais Magufuli kuwaondolea wachimbaji hao baadhi ya kodi ambazo zilikua kero kwao na zilizosababisha wachimbaji hao kutopata faida na biashara hiyo. Mkuu wa wilaya hiyo, Maryprisca Mahundi amepongeza maamuzi hayo ya Raii na kueleza kuwa, hali hiyo inaleta matumaini hasa wachimbaji hao ambao wamekuwa wakishindwa kukidhi mahitaji yao.

Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo mkoani humo, Leonard Manyesha amesema wamefurahishwa na maamuzi hayo na kueleza kuwa wapo tayari kufuata maagizo Rais aliyotoa wakati alipofanya mkutano na wachimbaji jiji Dar es salaam.

“Tumekuwa tukichimba madini, lakini faida hakuna kutokana na mrundikano wa kodi, sasa Rais wetu ametusikia na ameamua kutuondolea kodi hizo, hatuna uwezo wa kuandamana hadi Dar es salaam, hivyo tumeona tufikishe salamu zetu kupitia kwa Mkuu wa Mkoa”. Amesema Manyesha.

Mbunge wa jimbo la Lupa, Victor Mwambalaswa, amesema dhumuni la bunge kupitisha Sheria hiyo ya madini ni kwa sababu wameona kuna umuhimu wa wachimbaji hao kunufaika zaidi na hivyo kuwataka kutumia fursa hiyo ipasavyo ili kuleta maendeleo.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Sophia Kumbuli, amesema mabadiliko hayo yatawaletea maendeleo wachimbaji hao na mapato yataongezeka.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter