Home VIWANDA Manyara yajipanga kuvuka malengo uanzishaji viwanda

Manyara yajipanga kuvuka malengo uanzishaji viwanda

0 comment 58 views

Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amesema mkoa huo umetekeleza agizo la kila mkoa kuanzisha viwanda 100 lilitolewa na Waziri wa TAMISEMI, Suleiman Jafo. Mkuu huyo amesema hayo wakati wa ziara ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan wilayani Hanang na kueleza kuwa hadi kufikia Septemba 30 mwaka huu, kulikuwa na viwanda vipya takribani 29, baadhi vikiwa vimekarabatiwa na vinafanya kazi, huku vingiwe vikiwa katika hatua za ujenzi na baadhi vikiwa bado havijaanza ujenzi.

Mnyeti ameeleza kuwa wanatarajia mkoa huo kufikia na kuvuka malengo ya viwanda vipya zaidi ya 100 kabla ya mwezi Desemba mwaka huu na kuongeza kuwa ofisi yake inaendea na jitihada za kuhamasisha wananchi kuwekeza katika viwanda ili kukuza uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla.

“Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2013 za Ofisi ya takwimu ya taifa zinaonyesha kuwa mkoa wa Manyara una viwanda 2,400 kati ya hivyo viwanda vidogo sana ni 2,067 vidogo 305, vya kati 14 na vikubwa 14”. Amesema Mkuu huyo wa mkoa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter