Home BIASHARA Wafanyabiashara Zanzibar kubanwa

Wafanyabiashara Zanzibar kubanwa

0 comment 123 views

Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar, Hassan Khamis Hafidh amesema serikali ya Zanzibar itachukua hatua kali kwa wafanyabiashara watakaobainika kuingiza bidhaa zisizo na viwango. Naibu Waziri Hafidh amesema hayo akiwa katika Bandari ya Malindi na kuongeza kuwa, ni jukumu la serikali kulinda afya za wananchi hivyo bidhaa yoyote ambayo sio salama kwa matumizi ya wananchi haitaruhusiwa ili kuepusha madhara yoyote yanayoweza kutokea.

Aidha, kiongozi huyo amewataka wafanyabiashara kufanya shughuli zao kwa kuzingatia Sheria na kuwasisitiza waache mazoea ya kununua bidhaa kwa bei nafuu ili kupata faida pasipo kuzingatia ubora.

Akiwa bandarini hapo kushuhudia zoezi la kuhamisha tani 520 za sukari kuelekea mashimo ya mchango yaliyopo kijiji cha Zingwezingwe baada ya kugunduliwa kuwa sukari hiyo haina viwango vinavyotakiwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu, Naibu huyo ameweka wazi kuwa ulinzi na usalama umeimarishwa kuhakikisha zoezi hilo linamalizika.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Chakula na Dawa, Dk. Khamis Ali Omar amesema mwaka jana, makontena takribani 20 ya sukari yenye uzito wa tani 520 ambayo ni mali ya kampuni ya Rashid Ali Trader yaliingizwa Zanzibar na baada ya uchunguzi iligundulika kuwa haina kiwango.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter