Home BIASHARA Wanaofunga upya sukari waonywa

Wanaofunga upya sukari waonywa

0 comment 65 views

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Dk. Ngenya Athuman ametoa onyo kwa wafanyabiashara wenye tabia ya kufungasha upya sukari kutoka nje kwa kutumia mifuko ya wazalishaji wa ndani. Dk Athuman ametoa onyo hilo jijini Dodoma wakati akiongoza timu ya wataalamu kufanya ukaguzi wa bidhaa ya sukari katika maduka ya soko la majengo jijini humo.

“Tumepata taarifa za kuwepo wafanyabiashara ambao sio waaminifu, wamekuwa wakifungasha upya sukari kutoka nje ya nchi kwenye vifungashio vya wazalishaji wa ndani, tukiwabaini hatutakuwa na huruma nao, jambo hili halikubaliki. Tunachokifanya sasa ni kuchukua sampuli hizi za sukari na kwenda kupima kuangalia kama zinakidhi vigezo na viwango vya ubora vya Tanzania, kama matokeo yataonesha hazina ubora tutatafanya utaratibu wa kuziondoa sokoni, tutakwenda Bodi ya sukari watubainishie wale waliowapa vibali vya kuingiza sukari, ili tuwachukulie hatua wale ambao watabainika kuwa wameingiza sukari isiyo ya viwango”. Ameeleza Mkurugenzi huyo.

Kwa mujibu wa maelezo ya Dk. Athuman, wafanyabiashara hao wamekuwa wakiingiza sukari hiyo kutoka Msumbiji, Brazil na Thailand.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter