Home BIASHARA Wateja Fastjet waanza kurudishiwa nauli

Wateja Fastjet waanza kurudishiwa nauli

0 comment 127 views

Msemaji wa Shirika la ndege la Fastjet Tanzania Lucy Mbogoro amesema shirika hilo limeanza kurejesha nauli za wateja walionunua tiketi baada ya kusitisha safari zake. Fastjet imechukua hatua hiyo baada ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kuliagiza shirika hilo kuwarudishia fedha abiria wote waliokata tiketi au kuwatafutia nafasi za safari katika mashirika mengine ya ndege.

Mbogoro amesema baadhi ya wateja wao hasa wale walionunua tiketi kupitia mtandao wameanza kurudishiwa fedha hizo kuanzia Jumatatu wiki hii.

“Jumatatu tulitoa tangazo kuwa tutaanza kushughulikia malipo ya wateja wetu pamoja na wadau wengine tunaofanya nao biashara, siku hiyo hiyo tulianza kushughulikia kwa wale walionunua kwa M-Pesa, Airtel Money na Tigo Pesa. Ila kwa wale walionunua kwa ‘cash’ tulitangaza tutaanza kushughulikia malipo yao tarehe 20 na tayari tumeanza kulishughulikia hilo, tumekuwa tukiendelea na taratibu za benki kwa sababu hatuwezi kukaa na fedha nyingi, lazima tuzipeleke benki”. Amesema Msemaji huyo.

Aidha, Mbogoro amesema katika kurudisha fedha hizo, watatoa kipaumbele kwa wateja waliotarajia kusafiri kuanzia Desemba 20 hadi 31, mwaka huu ili kuwawezesha kuendelea na shughuli zao. Wale wanaotarajiwa kusafiri kuanzia Januari 2019 wataendelea kulipwa taratibu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter