Home Elimu Maandalizi ujenzi chuo cha TEHAMA waanza

Maandalizi ujenzi chuo cha TEHAMA waanza

0 comment 211 views

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imesema maandalizi ya ujenzi wa chuo mahiri cha TEHEMA utakaofanyika katika eneo la Nala Dodoma yameanza rasmi Januari 29, 2024.

Taarifa ya Wizara hiyo inasema Wizara inatekeleza miradi miwili ya ujenzi wa Vyuo vya TEHEMA katika jiji la Dodoma na eneo la Buhigwe mkoani Kigoma.

Wizara inaleza kuwa chuo hicho cha Nala kitakuwa kinatoa mafunzo ya ujuzi kwa vijana na wabunifu nchini kuhusu masuala ya TEHAMA kama vile Teknolojia zinazoibukia (Emerging Technologies) Usalama wa Mifumo ya Mawasiliano pamoja na utengenezaji wa mifumo ya TEHAMA.

“Chuo hiki kitakuwa tofauti na vyuo vingine kwa kuwa ni chuo ambacho kitakuwa kinatoa mafunzo kwa muda mfupi kwa njia ya moduli kulingana na mahitaji kwa nyakati husika .

Baada ya moduli kuisha, mhitimu atakuwa amepewa ujuzi kwenye eneo mahususi na kumwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na tija. Hii itapelekea vijana wengi kujiajiri au kuajiariwa katika sekta ya TEHAMA kulingana na mahitaji,” inaeleza taarifa hiyo.

Sambamba na hilo, Wizara imesema imeweka mpango wa ufadhili wa mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa watumishi wa umma 500 ambapo awamu ya kwanza wanafunzi ishirini wamepata ufadhili wa mafunzo ya muda mrefu katika vyuo vikuu vya nje ya nchi.

Pia, Wizara imetenga nafasi kwa ajili ya wataalamu arobaini kwenye mafunzo ya muda mfupi nje ya nchi ambapo kati ya hao 15 ni maprofesa kutoka katika vyuo mbalimbali.

Imetaja vyuo hivyo kuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam maprofesa watano, Chuo Kikuu cha Dodoma watano pamoja na Mbeya University of Science and Technology watano.

Nafasi 15 zinatolewa kwa watumishi wa umma kutoka kwenye Taasisi mbalimbali ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mammlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na masomo ya Anga za Juu (Space Technology).

“Utekelezaji wa miradi hii ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa tatu wa Taifa wa Maendeleo wa mwaka 2021/2026 pamoja na wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020/2025 ambayo inasisitiza uwepo wa mafunzo ya ujuzi na ubunifu katika TEHAMA nchini.

Ujenzi wa vyuo hivyo utachochoa maendeleo katika wakati huu wa mapinduzi ya 4, 5 na 6 ya viwanda ambayo ndiyo chachu ya ukuaji wa uchumi wa kidigitali duniani,”inasema taarifa hiyo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bw. Mohammed Khamis Abdulla akitoa ufafanuzi kwa washauri elekezi kutoka Korea walipokuwa wakitembelea eneo la Nala, jijini Dodoma.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa utekelezaji wa mradi huo unagharamiwa na Serikali ya Tanzania kwa kuwezesha upembuzi yakinifu pamoja na uandaaji wa mitaala na miongozo ya chuo hicho.

Fedha zitakazotumika kujenga chuo hicho ni mkopo wa masharti nafuuu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Korea kupitia Exim Benki ya Korea.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter