Home VIWANDAMIUNDOMBINU Mwenyekiti wa Mbinga Mji ataka miradi ya milioni 232 ikamilishwe

Mwenyekiti wa Mbinga Mji ataka miradi ya milioni 232 ikamilishwe

0 comment 264 views

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Kelvin Mapunda ametoa siku 10 kwa mafundi wanaotekeleza miradi ya bakaa kukamilisha kazi yao na kukabidhi kwa Halmashauri.

Agizo hilo lilitolewa Januari 29, 2024 wakati wa ziara yake ya kukagua miradi sita ya bakaa yenye thamani ya jumla ya Shilingi milioni 232.

“Ninatoa siku 10, kuanzia Januari 30 miradi yote ya bakaa ambayo haijakamilika, ikamilike,” amesema Mapunda.

Tafsiri yake ni kwamba miradi yote inatakiwa ikamilike kabla au ifikapo Februari 8 mwaka huu.

Miradi ambayo Mapunda alitembelea ni ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya Msingi Mbinga yenye thamani ya Sh. milioni 60, madarasa mawili katika shule ya Msingi Mateka yenye thamani ya Sh. milioni 40 na madarasa mawili katika Shule ya Msingi Myangayanga yenye thamani ya Sh. milioni 40.

Miradi mingine ni ujenzi wa shule mpya ya msingi Lusewa, madarasa mawili na ofisi moja (milioni 26), madarasa mawili katika shule ya msingi Beruma, kata ya Betherehemu (milioni 26) na madarasa mawili katika Shule ya Msingi Utiri (Milioni 40).

“Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais shupavu Dkt. Samia Suluhu Hassan ilitoa pesa kwaajili ya kutekeleza miradi hii. Hivyo basi, tunapaswa kutekeleza miradi hii kwa wakati na ubora wa hali ya juu,” amesema Mapunda.

Amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kuwasogezea wananchi huduma za kijamii.

Baadhi ya miradi ya bakaa inayotekelezwa Halmashauri ya Mji wa Mbinga.

Baadhi ya miradi ya bakaa inayotekelezwa Halmashauri ya Mji wa Mbinga.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Betherehemu alimshukuru Mwenyekiti kwa miradi hiyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter