Home Elimu Maandiko ya kisasa yatavutia utalii: Naibu Waziri Kitandula

Maandiko ya kisasa yatavutia utalii: Naibu Waziri Kitandula

0 comment 126 views

Kuwepo kwa maandiko ya kisasa yanayoendana na hali halisi ya biashara ya utalii duniani kutawezesha kukuza biashara ya utalii nchini na kuvutia wawekezaji.

Naibu Waziri wa maliasili na Utalii Dunstan Kitandula ameeleza hayo wakati akiongea na uongozi na watumishi wa Chuo cha Utalii Kampasi ya Arusha (NCT) Tanzania.

Kitandula amesema kuwepo kwa maandiko ya kisasa yanayoshawishi na kuboresha biashara ya utalii kutakuza biashara hiyo na kuongeza mchango wa pato la taifa.

Amesema ili chuo hicho kiwe hai na kuonekana ni lazima kuwepo na maandiko ya kibiashara yanayoshawishi wafadhili au serikali kutoa fedha kwa ajili ya maendeleo ya chuo.
Kitandula amekipongeza chuo hicho kwa jitihada na hatua mbalimbali wanazochukua katika kuhakikisha chuo kinatoa wahitimu walio bora na waliopata mafunzo kwa vitendo katika uhalisia wa biashara ya utalii inayoendela duniani.

“Nawapongeza kwa ujenzi unaondelea katika eneo hili kwani kwa kufanya hivyo mtaongeza udahili wa wanafunzi katika fani mbalimbali zinazoendeshwa hapa chuoni,” amesema.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Florian Mtei ameushukuru uongozi wa Wizara kwa kuwa umekuwa karibu na Chuo katika kusaidia mambo mbalimbali kwa ajili ya Maendeleo ya Chuo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter