Kampuni ya upakuaji wa makontena katika bandari za Tanzania ‘TICTS’ imechangia mifuko ya saruji 1,200 na mabati 1,200 katika ujenzi wa hosteli ya wasichana katika Shule ya Sekondari ya Ilele wilayani mlele mkoani Katavi.
Hosteli hiyo inakadiriwa kutumika na wasichana takriban 200 itakapomalizika. Aliyekabidhi mchango huo ni Donald Talawa, Mkurugenzi wa maendeleo wa kampuni ya TICTS aliyeshuhudiwa na Bi. Rachel Kasanda, Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Bw Alexius Kagunze Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Mlele na Bw Deus Bundala, Mwenyekiti wa halmashauri ya Mlele.