Home Elimu UN yawapiga msasa washiriki wa tuzo ya Uwezo kuhusu SDGs

UN yawapiga msasa washiriki wa tuzo ya Uwezo kuhusu SDGs

0 comment 100 views

WANAFUNZI kutoka shule 100 za mkoa wa Dar es Salaam na Pwani wamekuwa wakishiriki katika mradi wa tuzo ya uwezo unaoendeshwa na  Great Hope Foundation ambapo mapema wikiendi hii kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa walifanya mafunzo ya malengo ya dunia (SDGs) yaliyoambatana na utoaji wa tuzo hizo kwa vijana zaidi ya 100 kutokea shule tofauti.

Mradi huo ulioanza miaka minne iliyopita umelenga kuwawezesha wanafunzi kutambua vipaji vyao na kushiriki katika mafunzo ya ujasiriamali.

Aidha mradi huo umetengeneza jukwaa la kumfanya mwanafunzi atambue kwamba elimu ya ujasiriamali ni sehemu ya mafunzo ya kuwezesha ushiriiki wa kuleta maendeleo kwa mujibu wa malengo endelevu ya Umoja wa Mataifa.

Malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa yana vipengele 17 ambavyo ushiriki wa vijana ni muhimu.

Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC), Didi Nafisa alisema kwamba mradi huo ni sehemu ya miradi yenye lengo la kutoa mafunzo mbalimbali ikiwamo matumizi ya ubunifu wa kujiongeza katika ujasiriamali.

Ofisa habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa(UNIC), Didi Nafisa akielezea utekelezaji wa malengo 17 ya dunia (SDGs) wakati wa mafunzo ya SDGs yalioendeshwa na Great Hope Foundation kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa yaliyoambatana na utoaji wa tuzo ya uwezo kwa vijana zaidi ya 100 kutokea shule tofauti katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa shule ya sekondari Makongo jijini Dar es Salaam.

Alisema katika miradi ya Umoja wa Mataifa,  vijana waliofikiwa mpaka sasa ni 60,000 na ambapo wengine wamekuwa wakiendesha miradi ya ufugaji, ujasiriamali, ufyatuaji matofali, na utengenezaji wa vifungashio.

Naye Mratibu wa Kitaifa wa Mradi katika taasisi ya Great Hope, Noelle Mahuvi alisema katika mahojiano kwamba mafunzo hayo ni msaada mkubwa kwa vijana katika kujitambua na kuona kwamba kazi za nje zina mchango mkubwa wa maendeleo.

Mratibu wa Kitaifa wa Mradi katika taasisi ya Great Hope, Noelle Mahuvi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mafunzo ya malengo ya dunia (SDGs) yalioendeshwa na Great Hope Foundation kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa yaliyoambatana na utoaji wa tuzo ya uwezo kwa vijana zaidi ya 100 kutokea shule tofauti katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa shule ya sekondari Makongo jijini Dar es Salaam.

Alisema wamekuwa wakishirikiana na UNDP katika kuwaelimisha vijana na kuwasaidia katika kusukuma mbele maendeleo kwa kutumia elimu ya ujasiriamali.

Alisema kutokana na mafunzo hayo vijana walioingia chuo kikuu wamekuwa chachu ya wenzao ya kujua manufaa ya ujasiriamali yaani wakiendelea kujifunza darasani na kujifunza nje.

Naye Nancy Faustine mmoja wa wanufaika wa mradi huo kutoka Shule ya sekondari Zanaki amesema kwamba wamefurahishwa na mafunzo kwani yamewezesha wao kurekebisha kantini yao kwa kuipaka rangi na kutengeneza bidhaa za utamaduni na kuziuza.

Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Zanaki, Nacy Faustine aliyeshiriki na kuibuka mshindi wa mradi wa Uwezo Awards unaoendeshwa na Great Hope Foundation nchini akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushiriki wake na jinsi alivyonufaika na mradi huo wakati wa mafunzo ya malengo ya dunia (SDGs) yalioendeshwa na Great Hope Foundation kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa yaliyoambatana na utoaji wa tuzo ya uwezo kwa vijana zaidi ya 100 kutokea shule tofauti katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa shule ya sekondari Makongo jijini Dar es Salaam.

Alisema mafunzo waliyopewa kupitia tuzo ya uwezo yanatoa mwanga wa kujielewa miongoni mwa vijana na kutambua ushiriki wao katika malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu.

Alisema kupitia mradi huo walipata nafasi ya kuchukuliwa na TANAPA na kutembelea misitu ya Magamba na kutambua  ulinzi wa mazingira kama sehemu ya lengo la maendeleo endelevu.

Alisema Uwezo Award ni moja ya nyenzo muhimu ya kufundisha kujitambua kwa wahitaji.

Wanafunzi wa shule za Dar es Salaam na Pwani walioshiriki mafunzo ya SDGs yalioendeshwa na Great Hope Foundation kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa yaliyoambatana na utoaji wa tuzo ya uwezo kwa vijana zaidi ya 100 kutokea shule tofauti katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa shule ya sekondari Makongo jijini Dar es Salaam.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter