Home FEDHA Mapato ya TRA yaongezeka

Mapato ya TRA yaongezeka

0 comment 122 views

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema makusanyo ya kodi yameongezeka kutoka Sh. 14.4 trilioni ya mwaka 2016/2017 hadi Sh. 15.5 trilioni kwa mwaka wa fedha 2017/2018. Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA Richard Kayombo amesema moja ya sababu ya ongezeko hilo ni elimu ya kodi kuzidi kueleweka kwa walipakodi na wananchi.

Kayombo pia amebainisha kuwa ukaribu wa mamlaka hiyo na walipakodi umesaidia ongezeko la mapato kwa kiasi kikubwa kutokana na kutoa fursa kwa changamoto mbalimbali kutatuliwa na kuongezeka kwa walipakodi wapya.

Katika kipindi cha Julai 2017 hadi Juni 2018, TRA imefanikiwa kukusanya takribani Sh. 15.5 trilioni ikilinganishwa na Sh. 14.4 ya mwaka uliopita, kiasi ambacho ni ongezeko la sawa na asilimia 7.5

Kayombo ameweka wazi kuwa, fedha zinazokusanywa na mamlaka hiyo zinatumika katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara na reli pamoja na upatikanaji wa elimu na afya bora na mambo mengine ambayo ni muhimu kwa watanzania.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter